Header Ads Widget

TIMU YA NETIBOLI YA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAFUZU HATUA YA ROBO FAINAL KWA MARA YA KWANZA**

Timu ya netiboli ya Wizara ya Maliasili na Utalii leo Septemba 27,  2024 imeandika historia kwa kufuzu kwa mara ya kwanza hatua ya  robo fainali  ya Mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Idara na Wizara za Serikali (SHIMIWI) yanayoendelea kufanyika  Mkoani Morogoro.


Ushindi huo umepatikana  baada ya timu hiyo kuibamiza  timu ya  TAKUKURU goli 27 kwa 20 katika mchezo uliokuwa na ushindani mkali dhidi ya mahasimu hao  ambapo Wizara hiyo ilifanikiwa kuishinda timu hiyo na kuvunja mwiko wa kutokufuzu mashindano hayo tangu timu hiyo ilipoanza  kushiriki michuano hiyo ya SHIMIWI hadi kufikia sasa


Akizungumza mara baada ya ushindi  huo,  Kocha mahiri wa timu hiyo, Bi. Rahma Kilimba, ameipongeza timu hiyo kwa kuweka historia ya kipekee ya kufuzu hatua ya  robo fainali ya michuano hiyo  huku akisistiza kuwa wachezaji wake wana ari ya kutosha na anaimani timu hiyo itafika fainali ya michuano na hata kuchukua ushindi katika michuano hiyo


 "Ni siku ya kihistoria kwetu kufuzu robo fainali kwa mara ya kwanza. Tumefanya kazi kwa bidii na tunafurahia kufika hapa. Tunatumai kuwa tutashinda robo fainali na hatimaye kufika fainali katika michuano hii kwa sababu ari ya kufika huko tunayo" amesema Rahma.


Kwa upande wake Mchezaji wa timu hiyo, Asha Kitungo  amesema wao kama wachezaji wanaimani kubwa ya kufanya vizuri zaidi huku akitoa sifa kede kede kwa Kocha wa Boli Rahma kwa kuwafunda na hatimae kufika hatua hiyo adhimu


Mratibu wa Michezo wa Wizara, Bi. Getrude Kassara ametumia fursa hiyo kuwapongeza wachezaji hao kwa kuendelea kuipeperusha Bendera ya Wizara ya Maliasli na Utalii huku akisisitiza kuwa hatua ya wao kufuzu ni jambo la kihistoria na  zuri la kupongezwa 


" Hongereni sana wachezaji wetu, mnaipeperusha vyema bendera ya Wizara ya Maliasili na utalii, tunawapongeza sana, hongereni kwa kuingia robo fainali, sula hili ni la kihistoria " alisema Kassara


Aidha, ameeleza kuwa uongozi mzima wa Wizara pamoja na uongozi wa timu ya Wizara  uko nyuma yao kwa kila hatua, hivyo waendelee kupambana na kuutangaza utalii kupitia michezo


Katika siku ya leo, Jumla ya michezo mitatu ya raundi ya 16 bora imechezwa kwa upande wa Wizara ambapo, Mchezo wa Netiboli na Kamba ( Me) Wizara imeibuka mshindi na kufuzu hatua ya robo fainali  huku kwa upande wa Kamba (ke) Wizara hiyo ilishindwa kusonga hatua ya mbele mara baada ya kupoteza mchezo wake  dhidi ya Wizara  ya Afya.






 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI