Mkuu wa mkoa wa Iringa Peter Serukamba na uongozi wa shule za Real Hope Mafinga wakiwa katika Picha ya pamoja na wahitimu wa awali ,Darasa na saba na kidato Cha nne shule za Real Hope Mafinga baada ya Mahafali iliyofanyika Jana shuleni hapo na mkuu wa mkoa kuwa Mgeni Rasmi picha na Matukio Daima App
Imeonyesha jinsi ushirikiano kati ya wazazi, walimu, na jamii unavyoweza kuleta mabadiliko chanya katika jamii yetu kupitia elimu.
Mwaka huu, shule hiyo imeendelea kuvuna matunda ya juhudi zake tangu ilipoanzishwa mwaka 2016, kwa idadi ya wanafunzi walioongezeka na mafanikio ya kitaaluma yaliyopatikana.
Uanzishwaji na Ongezeko la Wanafunzi
Shule ya Real Hope ilianza mwaka 2016 ikiwa na jumla ya wanafunzi 41.
Tangu wakati huo, shule imekuwa ikiongezeka kwa idadi ya wanafunzi, jambo linalodhihirisha ubora wa elimu inayotolewa. Hadi sasa, shule ina jumla ya wanafunzi 301, huku ikiwa imeshahitimu wanafunzi wa kidato cha nne mara tano na sasa ikiwa inatoa mahafali yake ya sita.
Mwalimu Geofrey Lukosi, aliyesoma risala ya shule hiyo, alieleza kuwa ongezeko la wanafunzi limechangiwa na kuboreshwa kwa mazingira ya elimu shuleni, ambayo yameleta mabadiliko chanya kila mwaka.
Mbali na ongezeko la wanafunzi, shule imeweza pia kutoa fursa za ajira kwa jamii inayozunguka.
Tangu kuanzishwa kwake, idadi ya wafanyakazi imeongezeka kutoka 13 hadi 27, ikijumuisha walimu wa masomo mbalimbali na wafanyakazi wasio walimu. Hii imeifanya shule kuwa na uwiano mzuri wa walimu kwa wanafunzi, jambo linalochangia ubora wa elimu inayotolewa.
Mafanikio ya Kitaaluma na Nidhamu Shule ya Real Hope Mafinga imedhihirisha mafanikio makubwa katika nyanja za kitaaluma.
Wanafunzi wa shule hiyo wamekuwa wakifanya vizuri katika mitihani mbalimbali ndani na nje ya shule.
Hii imeipa shule heshima kubwa, sio tu kwa wanafunzi bali pia kwa walimu na jamii nzima inayozunguka shule hiyo.
Mafanikio haya ni matokeo ya juhudi za walimu ambao wamejitolea kwa hali na mali kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bora.
Walimu wamekuwa wakitumia muda mwingi kutoa msaada wa kitaaluma, kuandaa mitihani, na kuwa karibu na wanafunzi katika safari yao ya kielimu.
Pia, nidhamu ni kipengele kingine muhimu ambacho kimeleta mafanikio katika shule ya Real Hope.
Wanafunzi wamefundishwa na kuhamasishwa kudumisha nidhamu ya hali ya juu, ambayo imewawezesha kuzingatia masomo na kufikia malengo yao.
Nidhamu hii imesaidia kuwafanya wanafunzi kuwa na mwelekeo sahihi wa kimaisha, si tu ndani ya shule, bali hata wanapokuwa nje ya mazingira ya shule.
Miundombinu na Mazingira ya Kujifunzia
Shule ya Real Hope Mafinga imewekeza sana katika miundombinu bora ya kufundishia na kujifunzia. Mwalimu Lukosi alieleza kuwa shule ina miundombinu ya kutosha, ikijumuisha madarasa, mabweni, maabara, vyoo, na kumbi za mikutano. Miundombinu hii inawawezesha wanafunzi kusoma katika mazingira mazuri, jambo linalochangia kuongeza ari ya kujifunza na kufundisha.
Vilevile, shule imeboresha huduma zake kwa wanafunzi kwa kutoa chakula bora, ikiwemo mlo wa chai na vitafunwa, pamoja na milo yenye virutubisho kama samaki, dagaa, mayai, na maziwa.
Huduma hizi zimeifanya shule kuwa kivutio kwa wazazi, ambao wameendelea kuwaleta watoto wao kupata elimu bora katika shule hiyo.
hali ya taaluma katika shule yetu ni nzuri na imekuwa ikikua siku hadi siku tangu mwaka 2019 shule ilipotoa kidato cha nne kwa mara ya kwanza.
Kwa mwaka jana hali ya matokeo ya taaluma ilikuwa kama ifuatavyo kwa kidato cha pili mtihani wa taifa, tulikuwa na jumla ya wanafunzi 53 ambapo katika hao wanafunzi 51 walipata daraja la kwanza(yaani Division one), Na wanafunzi wawili pekee walipata division 2, kwa maana hiyo hatukuwa na divion three, four au zero, hii inamaanisha kwamba wanafunzi wote walipata ufaulu bora.
Kwa kidato cha nne mtihani wa taifa wa mwaka jana, tulikuwa na jumla ya wanafunzi 40 ambapo katika hao wanafunzi wote 40 walipata daraja la kwanza(yaani Division one), kwa maana hiyo hatukuwa na division two, three, four au zero hii inamaanisha kwamba wanafunzi wote walipata ufaulu bora, na wote wamepangwa katika shule za A-LEVEL na vyuo mbalimbali.
Leo hii kuna jumla ya wahitimu 54 wa kidato cha nne ambao pia wamekuwa wakifanya majaribio na mitihani mbali mbali kwa ajili ya kuwaandaa vyema kwa mtihani wao wa mwisho wa taifa utakaoanza tar 11/11/2024. Kama sehem ya
Changamoto na Mikakati ya Kuzishinda
Licha ya mafanikio makubwa yaliyopatikana, shule ya Real Hope Mafinga haijakosa changamoto.
Idadi ya wanafunzi wa kidato cha nne imepungua kutoka 61 hadi 54 kutokana na changamoto za kiafya na matatizo ya kifamilia ambayo yamewalazimisha baadhi ya wanafunzi kukatisha masomo yao.
Hata hivyo, uongozi wa shule umeweka mikakati ya kuhakikisha changamoto hizi zinashughulikiwa kwa kuwapa wanafunzi usaidizi wa karibu na kuwashauri ili waweze kuendelea na masomo yao bila kukatizwa.
Aidha, suala la ada na tozo mbalimbali liliibuliwa na wanafunzi wakati wa mahafali yao.
Walimu na wanafunzi walieleza kuwa ingawa shule inatoa huduma bora, kuna haja ya serikali na wadau wa elimu kuangalia upya ada za mitihani na tozo nyingine ili kupunguza mzigo kwa wazazi. Wanafunzi walipendekeza kuwa shule binafsi kama Real Hope zinatoa mchango mkubwa katika kukuza elimu nchini, hivyo zinastahili kupewa unafuu wa gharama.
Ushirikiano wa Wazazi na Jamii
Mafanikio ya shule ya Real Hope yamewezeshwa kwa kiasi kikubwa na ushirikiano mzuri kati ya walimu, wanafunzi, na wazazi.
Wazazi wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha watoto wao wanapata elimu bora kwa kuwapa mahitaji yote muhimu ya shule na kulipa ada kwa wakati.
Pia, wazazi wamekuwa wakiunga mkono juhudi za walimu na uongozi wa shule, jambo ambalo limeleta umoja na mafanikio makubwa.
Katika risala yao, wanafunzi walitoa shukrani zao za dhati kwa wazazi na walezi wao kwa kujitoa muhanga ili kuwapatia elimu. Walisema, "Tunawapenda sana wazazi na walezi wetu," na kuahidi kuendelea kuwaombea kwa Mungu ili wawe na afya njema na mafanikio zaidi.
John Kalinga na Sara Sanga ni wazazi wa wanafunzi wa Shule za Real Hope Mafinga wameipongeza shule hiyo kwa kutoa elimu bora na mazingira mazuri ya kujifunzia.
Wakizungumza katika mahafali ya shule hiyo, wazazi wamesema shule imeonyesha ubora katika nyanja za kitaaluma, nidhamu, na huduma kwa wanafunzi. Pia wamesifu juhudi za walimu na uongozi wa shule kwa kuhakikisha watoto wanapata malezi bora na elimu inayowaandaa kwa maisha ya baadaye.
Wazazi wameahidi kuendelea kushirikiana na shule kuhakikisha mafanikio zaidi yanapatikana na kuwahimiza wengine kuleta watoto wao kupata elimu Real Hope.
Mkurugenzi wa Shule na Jitihada Zake
Mkurugenzi wa shule ya Real Hope Mafinga, Dickson Mwipopo, amepewa heshima kubwa na wanafunzi na walimu kwa mchango wake mkubwa katika kuboresha mazingira ya elimu.
Mwipopo amepewa sifa kwa kuwaongoza wanafunzi na walimu kwa mfano, akiweka juhudi kubwa katika kuhakikisha shule ina miundombinu bora na huduma nzuri kwa wanafunzi. Wanafunzi walimpongeza kwa jitihada zake za usiku na mchana katika kuhakikisha shule inakuwa mahali bora pa kujifunza.
Wanafunzi walisema kuwa wamefurahia sana kusoma katika shule hiyo na wanatamani kila mwanafunzi angepata fursa ya kusoma katika shule za Real Hope kutokana na huduma nzuri zinazotolewa. Kwa upande wa walimu, walieleza kuwa Mkurugenzi Mwipopo ameonyesha uongozi bora ambao umechangia mafanikio ya shule kwa kiasi kikubwa.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Peter Serukamba, ameipongeza Shule ya Real Hope Mafinga kwa kutoa elimu bora na kuwa mfano wa kuigwa katika mkoa.
Akizungumza kwenye mahafali ya shule hiyo, Serukamba alisifu jitihada za uongozi na walimu kwa kuandaa mazingira bora ya kujifunzia.
Pia, alieleza kuwa serikali itaendelea kuwekeza katika sekta ya elimu ili kuhakikisha kila mtoto anapata nafasi ya kujifunza kwenye mazingira yanayofaa.
Aliwahimiza wanafunzi kuzingatia masomo yao na kuwataka wazazi kuendelea kushirikiana na serikali na taasisi binafsi kuinua viwango vya elimu nchini.
Hitimisho
Shule ya Real Hope Mafinga ni mfano wa jinsi taasisi za elimu binafsi zinavyoweza kuchangia maendeleo ya elimu nchini. Kupitia ushirikiano wa uongozi, walimu, wazazi, na jamii, shule imeendelea kuvuna mafanikio katika nyanja za kitaaluma, nidhamu, na maendeleo ya miundombinu.
Huku ikijipsnga kuwa shule itakayokuwa kwenye nafasi 10 Bora nchini kwani shule imeonyesha dhamira ya kuzishinda shule nyingine na kuendelea kuwa kivutio kwa wazazi na wanafunzi.
Kwa pamoja, wanafunzi, walimu, na wazazi wameweka msingi imara wa kuhakikisha elimu bora inapatikana kwa kila mtoto anayesoma katika shule hiyo.
Jitihafa za shule za Real Hope Mafinga wilayani Mufindi mkoani Iringa zinakwenda Sanjari na sera ya Taifa ya Elimu nchini Tanzania ambayo inalenga kutoa mfumo bora wa elimu unaokidhi mahitaji ya kijamii, kiuchumi, na kisiasa kwa maendeleo ya nchi.
Sera hii inazingatia kutoa fursa sawa za elimu kwa watoto wote, bila kujali jinsia, hali ya kiuchumi, au mazingira wanayotoka. Imeweka msingi wa kuhakikisha elimu ya msingi ni ya lazima na inapatikana bila malipo kwa watoto wote, huku ikisisitiza ubora wa elimu kwenye ngazi zote za masomo.
Aidha, sera inazingatia kuimarisha elimu ya sekondari na vyuo kwa lengo la kuzalisha wataalamu na nguvu kazi yenye ujuzi wa kisasa.
Serikali imeweka mikakati ya kuboresha miundombinu ya shule, kuongeza idadi ya walimu wenye sifa, na kuhakikisha upatikanaji wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia.
Kwa kuongezea, sera hii inalenga kuleta ushirikiano kati ya sekta binafsi na serikali ili kuimarisha ubora wa elimu nchini na kuongeza fursa za ajira kwa wahitimu.
Kumbuka iwapo unahitaji kusomesha Mwanao chagua shule za Real Hope Mafinga Kwa upande wa shule ya Msingi kuanzia awali piga simu 0748129999 au 0752599315 na Sekondari piga 0757444334 FOMU ZINAPATIKA KATIKA APP YA MATUKIO DAIMA AMA BONYEZA LINK HII FOMU ZA KUJIUNGA NA SHULE ZA REAL HOPE HIZI HAPA
0 Comments