Header Ads Widget

POLISI YAPIGA MARUFUKU MAANDAMANO YA CHADEMA



Na Matukio daima App,


Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini DCP David Misime amewatahadharisha wananchi kutojihusisha na maandamano yanayopangwa kufanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akisema maandamano hayo ni haramu.


Akizungumza leo na waandishi wa habari katika chuo cha Polisi Moshi, Mkoani Kilimanjaro, Msemaji wa jeshi la polisi David Misime amesema yeyote aliyepanga kusafiri kwa nia ya kushiriki maandamano hayo asitishe kwani watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.


Misime amewataka wananchi wa Dar es Salaam ambako maandamano hayo yamepangwa kufanyika kuendelea na shughuli zao na kuliachia jeshi kuendelea na uchunguzi dhidi ya matukio yanayoendelea ikiwa ni pamoja na utekaji wa watu, na watu kupotea na baadaye kubainika wamedhurika ama kuuawa.


Aidha jeshi limesema linawashangaa chama hicho kutaka kuwatoa kwenye reli ya kufanya uchunguzi baada ya kuagizwa na rais Samia Suluhu Hassan


“Kufanya maandamano ni kuvuruga amani ya Nchi yetu, tunatoa onyo kwa yeyote atakayeingia barabarani tutakabiliana naye kwa mujibu wa sheria za Nchi” amesema Misime.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI