NA. THABIT MADAI, ZANZIBAR- MATUKIO DAIMA APP
NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Dotto Mashaka Biteko amevitaka vitengo vya tathmini na ufuatuliaji Serikalini kuacha kufanya kazi kwa onyonge badala yake wajiamini na kuhakikisha fedha zinazotolewa na serikali kutekeleza miradi zinaleta matokeo chanya.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dk Doto Biteko wakati wa kufunga kongamano la tatu la Kitaifa la wiki ya ufuatiliaji, Tathmini na kujifunza hafla ambayo ilifanyika katika ukumbi wa golden tulip uwanja wa ndege Zanzibar.
Alisema watathmini hao ni vyema kuendelea kufanya kazi zao kwa kajiamini, na wasiwe wanyonge ili kuona kazi zinafanyika ikiwemo kufanya shughuli mbali mbali za kitaifa.
Hivyo, alisema wanataaluma wa tathmini na ufutiliaji sifa yao sio kumfurahisha mtu bali kumfanya mtu ajione alivyo na kumpa mbadala namna gani anaweza kufanya ili aboreshe kazi yake na kuwa na matokeo mazuri.
Katika hatua nyingine Majaliwa ametoa maagizo matano ikiwa ni pamoja na kuiagiza Wizara ya Sera na Uratibu wa Bunge, Ikamilishe mapema mfumo wa ufuatilaiji na tathmni na kuwezesha taarifa za utendaji wa serikali kupatikana kwa urahisi.
Pia Tume za Mipango zikamilishe uchambuzi wa miradi yote inayotekelezwa ndani ya serikali na kila mwaka kutoa taarifa ya utekelezaji wake itawezesha serikali kuona tija ya miradi hiyo iliyohidhinishiwa fedha nyingi.
Naye Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, sera, Bunge na Uratibu William Lukuvi amesema Serikali imeendelea kuchukua hatua kuhakikisha masuala ya tathmini na ufuatiliaji yana imarika.
Amesema hali hiyo imeleta mabadiliko kwani unakuwepo na uwajibikaji na uwazi.
Naye Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar, Juma Makungu Juma amesema wanatakiw akuwa na ajenda ya pamoja ili kuleta ufanisi katika utendaji kazi.
Kongamano hilo la siku nne, limewashirikisha watunga sera, watekelezaji wa sera, mashirika binafsi na serikali kutoka mataifa 12.
0 Comments