Header Ads Widget

MILIONI 385.5 KUWAWEZESHA WANANCHI KASULU KUPATA MAJI SAFI

 


Na Fadhili Abdallah,Kigoma



Utekelezaji wa mradi wa mfumo wa kutibu maji katika chanzo cha Mto Chai halmashauri ya mji Kasulu utawezesha wananchi wa kata sita za halmashauri hiyo  kunywa maji safi na salama na kuondokana na changamoto ya kunywa maji yenye tope.


Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mji wa Kasulu, Mhandisi Guttu Bundala akitoa taarifa  wakati mwenge wa uhuru ulipokuwa ukiweka jiwe la msingi katika mradi huo uliofanwa na kiongozi wa mwenge wa uhuru mwaka 2024, Godfrey Mnzava alisema kuwa kiasi cha shilingi milioni 385.5 kilichotolewa na serikali kutawezesha kutekelezwa kwa mradi huo. 

 

Bundala alisema kuwa katika  kukamilika kwa mradi huo kutawezesha wananchi 52,527 wa kata hizo kunufaika na upatikanaji wa maji safi na salama sambamba na kuongeza upatikanaji maji katika mji wa Kasulu ambao unakuwa kwa kasi.

 


Akizungumza katika mradi huo Mbunge wa jimbo la Kasulu Mjini, Profesa Joyce Ndalichako alisema kuwa anamshukuru Raisi Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha kupatikana kwa fedha hizo na mradi kutekelezwa ambapo utaongeza upaatikanaji wa maji safi na salama kufikia asilimia 76 kutoka asilimia 57 iliyokuwepo miaka mitatu iliyopita.

 

Akiweka jiwe la msingi katika mradi huo Kiongozi wa mwenge wa uhuru 2024, Gofrey Mnzava ameipongeza serikali ya Raisi Samia kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya kukamilisha miradi ya wananchi hivyo ametoa wito kwa wakandarasi kuhakikisha miradi inakamilika na inatoa huduma kwa wananchi.

 

Akipokea mwenge huo wa uhuru kutoka wilayani Buhigwe ili kuanza kukimbizwa katika halmashauri ya mji wa Kasulu wilayani Kasulu mkuu wa wilaya hiyo, Kanali Isack Mwakisu alisema kuwa ukiwa katika halmashauri hiyo mwenge utakimbizwa kwa umbali wa kilometa 49 ukitembelea, kufungua, kukagua,kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi minane yenye thamani ya shilingi bilioni 2.3.

 



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI