Header Ads Widget

MBOWE ASEMA KIBAO ALIPIGWA SANA KABLA YA KIFO CHAKE


Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amesema uchunguzi (post mortem) uliofanywa kwenye mwili wa Ali Mohamed Kibao mbele ya mwanasheria wa Chadema, umebaini kwamba alipigwa sana na kumwagiwa tindikali.


Mbowe ameyasema hayo nje ya chumba cha maiti katika Hospitali ya Mwananyamala, ambako viongozi na wanachama wa chama hicho, waliweka kambi tangu asubuhi kwa ajili ya kufuatilia taarifa za kupatikana kwa mwili wa Kibao.


Kibao alikuwa ni Mjumbe wa Sekretarieti ya Chadema Taifa na Msaidizi wa Katibu Mkuu wa chama hicho ambapo siku chache zilizopita, ilidaiwa kwamba ametekwa na watu wasiojulikana akiwa ndani ya basi, akisafiri kutoka Dar es Salaam kuelekea Tanga.


Muda mfupi baadaye, ndipo zilipopatikana taarifa kwamba mwili wake umeokotwa katika Viwanja va NSSF, Ununio jijini Dar es Salaam na baadaye kwenda kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Mwananyamala.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI