Na. Mwandishi Wetu Lamadi.
MJI wa Lamadi ulitawaliwa shangwe na shamrashamra za Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM waliojitokeza kumsindikiza Mgombea wa Mteule wa Udiwani Kata ya Lamadi Mhe. Joseph Goryo.
Msafara huo ulisindikizwa na mamia ya wana CCM huku ukipambwa na Vijana wa bodaboda kuanzia katika Ofisi za CCM Kata ya Lamadi kuelekea katika Ofisi za Msimamizi msaidizi wa Uchaguzi Ngazi ya Kata.
Aidha, Goryo kwa sasa yupo mguu sawa kusubiria kipyenga cha kuanza kampeni na vyama vingine vya upinzani hiyo Agosti 28, 2025.
![]() |
Mgombea Udiwani Mteule wa CCM, Joseph Goryo (katikati) akikabidhiwa fomu ya Udiwani na Msimamizi msaidizi wa Uchaguzi Ngazi ya Kata Bw. Tumaini Ladislaus Kazoba |
Goryo amesema kuwa, amejiandaa kufanya kampeni za kishindo ikiwemo kumuombea kura Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Rais Samia Suluhu Hassan, pamoja na Mbunge wa Jimbo la Busega.
"Nitafanya kampeni za kipekee na za kisasa ndani ya Kata kuomba kura ya Udiwani. CCM ina mambo mengi ya kuwafanyia Wananchi wa Lamadi.
Lakini pia kubwa zaidi ni pamoja na kumuombea kura Mama yetu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ili apate Lamadi apate kura za kishindo." Amesema Goryo.
Pia ameongeza kuwa, atatumia fursa za kiuchumi katika Kata hiyo ikiwemo masuala ya Utalii, Uvuvi, na kilimo ili kuongeza ukuaji wa kiuchumi kwa Wananchi na Taifa kwa ujumla.
"Tutafanikisha fursa katika Sekta ya Utalii tuna pori la akiba na tupo jirani ya Hifadhi ya Serengeti.
Maana halisi ya kazi na utu, Lamadi tunaenda kujenga soko kuu la kisasa lakini pia stendi ya mabasi hii ni ahadi ya Rais Samia Suluhu Hassan na sie kama wasaidizi wake tunaenda kumsaidia kwa vitendo" amesema Goryo.
Lamadi ni miongoni mwa Kata zilizopo Wilaya ya Busega Mkoa wa Simiyu ambapo ni miongoni mwa miji mikuu ya kibiashara ikiwa imepitiwa pia na Ziwa Victoria, lakini pia pori la akiba la Kijereshi.
![]() |
Mgombea Udiwani Mteule wa CCM Kata ya Lamadi, Mhe. Joseph Goryo akiwa na fomu yake baada ya kukabidhiwa Agosti 18, 2025 |
0 Comments