TAZAMA FULL VIDEO BOFYA LINK HII
Mwenyekiti wa Halmshauri ya wilaya ya Chalinze Hassan Mwinyikondo ametoa siku sita kwa Mamlaka ya Maji Safi na maji taka DAWASA wilaya ya Chalinze kuhakikisha wanamaliza tatizo la kukosekana kwa maji katika halmashauri hiyo ikiwemo katika Kata ya Msoga.
Agizo hilo amelitoa wakati akihitimisha ziara ya kuhimiza maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa na vitongoji Kata ya Msoga kwenye mkutano Mkuu wa Kata ya Msoga ambapo kero ya ukosefu wa maji iliibuliwa mara nyingi na Wananchi kuliko kero zingine zinazowasilishwa na Wananchi wa Kata hiyo ili Wakuu wa idara husika watafutie ufumbuzi haraka.
Mwinyikondo amesema amekutana na kero mbalimbali za ukosefu wa maji katika halmashauri hiyo wakati akiwa kwenye ziara za kazi vijijini ambapo kero mbalimbali zipizosababisha ukosefu wa maji zimeibuliwa kwa wingi jambo ambalo linaweza kuwakwamisha ushindi CCM katika chaguzi mbalimbali zinazotarajia kuanza hivi karibuni.
Alisema DAWASA walichokosea ni kukata mabomba yaliyowekwa kwenye vioksi vya kuuza maji na kusababisha kukosekana kwa uhakika wa huduma ya maji ya Bomba kwa wananchi wa Halmshauri ya Chalinze.
"Tumepokea kero ya huduma ya maji katika Kata na vijiji vyote vya Chalinze tukiwa kwenye ziara zetu za kazi vijijini hivyo sekta ya maji Jimbo la Chalinze wanaweza wakatumaliza, bila kusimamia utekezaji wa madhubuti wa sekta ya maji wanaweza wakatumaliza" alisema.
Alifafanua kuwa kuna changamoto zingine zinasikitisha sana, yaani mkandarasi anawezaje kukabidhi kazi kabla utekezaji wa mradi wa kazi haujaisha?" Alihoji Mwenyekiti huyo wa Halmshauri ya Chalinze.
Hatahivyo Mwenyekiti huyo wa Halmshauri ya Chalinze aliomba Mkutano maalumu na Mameneja ya sekta ya huduma za maji wa DAWASA na Mamlaka ya Maji vijijini RUWASA ili wakae kujadiliana kwa pamoja waone chakufanya ili kumaliza kero hiyo ya huduma ya maji Chalinze kwa pamoja.
Aidha kijibu kero na changamoto hizo za Wananchi Afisa Maji wa DAWASA Kata ya Msoga Muhsini Msisi amekiri kuwepo kwa changamoto hizo na kusema tayari DAWASA wameshighilikia sehemu kubwa ya kero hizo ambapo kwasasa wapo katika hatua ya kujaza maji kwenye matanki Kisha wafungulie maji yawafikie Wananchi.
"Tunatarajia siku tatu hizi kuanzia leo (Jana) hadi jumanne ni kusubiria matanki ya maji ya Maeneo ya Kijiji cha Mazizi huko Kata ya Lugoba na Msoga yakijaa maji changamoto hiyo itakuwa imekwisha" alisema Msisi.
Mkutano huo pia ulitanguliwa na mkutano wa ndani wa Wana CCM ambapo Mwenyekiti huyo ambaye pia ndio Diwani wa Kata ya Msoga alihimiza umuhimu wa kufanyika vikao vya Chama na Jumuiya zake kujenga uhai wa Chama Cha Mapinduzi CCM hasa kipindi hiki kuelekea chaguzi za serikali za mitaa na vitongoji.
Aidha pia mkutano huo wa ndani wa Wana CCM alisisitiza umoja na mshikamano miongoni mwa Wana CCM ili kufanikisha ushindi kwa Wagombea wa CCM katika chaguzi mbalimbali zinazotarajia kuanza hivi karibuni nchini kote.
0 Comments