Header Ads Widget

MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR HEMED SULEIMAN ABDULLA AMEFUNGUA MASHINDANO YA MAJESHI MOROGORO

 



NA FARIDA MANGUBE, MOROGORO

Makamu wa Pili wa Rais wa  Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla  amefungua mashindano ya Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania (BAMMATA) kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.

Akizungumza kwenye ufunguzi huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla  amewataka wanachezo kutumi michezo katika kujipatia kipato na kuliwakirisha vyema Taifa  katika mashindano ya Kimataifa. 

Pia amesema michezo ni moja ya yenzo muhimu ya kudumisha na kuimarisha  mashirikiano mahala pakazi na kuongeza ufanisi wa utendaji kazi wao.

Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la wananchi Tanzania ( JWTZ) Luteni General Salum Haji Othuman amesema lengo la michezo hiyo ni kuinua vipaji vilivyopo kwenye majeshi nchini na kujiandaa kwajili ya michezo ya kimataifa inayofanyika kila mwaka.

Brigedia Jenerali Said Hamis Said ni Mwenyekiti wa baraza hilo, amesema michezo hiyo imeaanza kutimua vumbi rasmi leo Septemba 6,2024 na yanatarajiwa kufikia mwisho Septemba 15 ambapo mgeni ramsi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Michezo ya majeshi inaundwa na kanda nane ambazo ni Ngome iliyopo chini ya JWTZ na kanda nyingine ni polisi , magereza , uhamiaji , zimamoto na uokoaji , Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)  na kanda ya Idara Maalumu  ya Serikali ya Mapinduzi  Zanzibar.

Michezo itakayochezwa ni soka, netiboli, basketi kwa wanaume na wanawake, volleyball riadha wanaume na wanawake zikiwemo za mbio za kilometa 21.

Mingine ni mpira wa mikono, mirusho ,vishale (Darts) na mchezo wa shabaha kwa kutumia silaha za moto  ambayo  itafanyika kwenye viwanja vya wazi isipokuwa wa shabaha ambao utatumika katika  viwanja maalumu vilivyoandaliwa kutumia silaha hizo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI