Header Ads Widget

HALMASHAURI YA IRINGA DC YAPATA USHINDI MKUBWA MASHINDANO YA SHIMISEMITA MWANZA

 


HALMASHAURI ya wilaya ya Iringa Vijijini imefanikiwa kushinda vikombe vitatu kikiweno Cha ushindi wa kwanza katika mchezo wa Draft.

Katika mashindano hayo ya shirikisho la michezo serikali za mitaa Tanzania( Shimisemita ) yaliyoshirikisha timu 100 za Halmashauri nchini .

Pamoja na mchezo wa Draft kushika nafasi ya kwanza Halmashauri hiyo imekuwa ya pili kwa mchezo wa Basketball na mshindi wa tatu katika mchezo wa Pool table hivyo kujitwalia makombe Matatu .

Huku michezo mingine kama kuvuta kamba wanawake  ,Darts wanaume, Volleyball wanaume na mchezo wa Basketball wanawake walibaki kidogo kutwaa ubingwa baada ya kufanikiwa kuingia hatua ya nusu Fainali .

Robart Masunya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Iringa Vijijini 

Ushindi huu mkubwa ni heshima  kubwa kwa Walimu na Wachezaji wote 37 waliopo Mwanza pia heshima kubwa  kwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo inayoongozwa na  Dkt Robert Masunya ,mwenyekiti wa Halmashauri Stivin Mhapa pia ni heshima kwa mkuu wa wilaya ya Iringa Khery James na uongozi wa mkoa wa Iringa Chini ya RC Peter Serukamba mkoa wa Iringa umeandika historia .


Mdau wa maendeleo wa wilaya ya Iringa Sositenes Mbedule amekuwa msaada mkubwa kwa timu hii ya wilaya ya Iringa Vijijini kwani kabla ya kwenda kushiriki michezo hii aliiwezesha Vifaa vya michezo.

Stivin Mhapa mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa Vijijini 

Matukio Daima media tunawapongeza sana wanamichezo wote na tutazidi kuwaletea taarifa zaidi ya Wachezaji hawa 37 tunawatakia safari njema kutoka Mwanza kurejea mkoani Iringa Kituo chao Cha kazi .

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI