Na, Matukio Daima App,
Jamii ya Wahadzabe na Wagatoga ambao wamekuwa wakiendeleza utamaduni wao kwa miaka mingi, ikiwemo shughuli za uwindaji na maisha ya kula matunda, mizizi na aina mbalimbali za wanyama wa porini, wameaahidi kujitokeza na kushiriki shughuli zote za uchaguzi wa serikali za mitaa.
Wamesema hayo, baada ya serikali ya wilaya ya Karatu, mkoa wa Arusha kuwa tembelea na kuwashirikisha programu na mipango mbalimbali ya kijamii, kidemokrasia pamoja na kuwahasisha ushiriki wao kwenye kuamua mambo yao, kwa kuchagua na kuchaguliwa kwenye nafasi mbalimbali za Kiuongozi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Ndugu Juma Hokororo, amewatembelea wananchi hao wa kijiji cha Mang'ola na kutoa elimu kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa pamoja na kuhamasisha wananchi hao, kuweza kushiriki kwenye mchakato huo muhimu wa kidemokrasia.
"Nimekuja kuwaambia na kuwahamisha kushiriki kwenye kugombea nafasi mbalimbali za Uongozi. Tungefurahi kuwaona watu wa Jamii hii ya Kihadzabe kwenye nafasi mbalimbali za Uongozi. Twendeni tuhamasishane kugombea na tukachague viongozi wanaotufaa kwa maendeleo ya Mang'ola." Amesema Ndugu Hokororo
0 Comments