Na, Matukio daima App,
Kufuatia uwepo wa taarifa ya maandamano yaliyoitishwa na mwenyekiti wa Chadema na kupewa jina la maombolezo ya amani, jijini Dar es salaam, .Chama cha Demokrasia na Maendeleo - Chadema kimedai kuwa polisi wamemzuia mke wa Freeman Mbowe, Dkt. Lilian Mbowe, asipite kutoka nyumbani kwake Mikocheni, Dar es Salaam, kwenda kazini.
Taarifa hizo zimekuja wakati, Mwenyekiti wa chadema Freeman Mbowe ambaye pia ni mume wa Dkt. Liliani akiwa amekamatwa na jeshi la polisi kutokana na maandamano hayo.
0 Comments