Na Fatma Ally Matukio DaimaApp Dar
Wasanifu Majengo wametakiwa kutumia vizuri bunifu zao na kulinda michoro yao ili kufaidika na uwekezaji, huku pia wajasiriamali nao wakitakiwa kuongeza ubunifu katika vifungashio na mikebe ili kuzipa thamani bidhaa zao jambo litakalosaidia kuhimili ushindani kitaifa na kimataifa
Rai hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam, Ofisa Mtendaji Mkuu wa BRELA, Godfrey Nyaisa,wakati akifungia mkutano wa wadau uliolenga kujalidili kwa pamoja kupata maoni ya rasimu ya mkataba wa sheria ya kimataifa inayohusu Ulinzi wa maumbo bunifu na michoro.
Nyaisa amefafanua kuwa maoni hayo ya wadau watayawasilishwa kwenye mkutano wa Kideplomasia wa nchi Wananchama wa Shirika la Miliki Ubunifu Duniani (WIPO) ambapo Tanzania ni mwanachama utakaofanyika, Riyadh nchini Saudi Arabia kuanzia Nov. 11 hadi 22 mwaka huu.
Amesema kuwa mkataba wa WIPO wa Sheria ya Maumbo Bunifu unalenga kuweka utaratibu au mfumo wa Kimataifa wa Usajili na Ulinzi wa Maumbo Bunifu kwa nchi na Mashirika Wanachama, mfumo huu utawezesha uwasilishaji wa maombi ya ulinzi wa maumbo bunifu kupitia WIPO ambapo mwombaji ataweza kuwasilisha ombi moja na kuchagua nchi zaidi ya moja zitakazokuwa zimeridhia mkataba huo ambazo anahitaji kupata ulinzi wa ubunifu wake,” amesema.
Hata hivyo, amesema kuwa mfumo huo utaongeza wigo wa ulinzi katika nchi nyingi kwa mara moja badala ya nchi moja kwa moja ambazo mbunifu anahitaji kulinda ubunifu husika jambo linalosaidia kupunguza gharama na ugumu wa ulinzi wa bunifu hivyo kikao hicho ni muhimu kwa wadau kutoa maoni.
Ameongeza kuwa endapo sheria hiyo itapitishwa na Tanzania kuridhia ni dhahiri itatoa fursa na kuongeza wigo kwa wabunifu wa maumbo, michoro bunifu wa Kitanzania kusajili na kulinda kazi zao katika ngazi ya kimataifa na kukuza biashara zao jambo litakalosaidia kuweza kuhimili ushindani katika masoko ya ndani na kimataifa.
"Kulingana na ushindani uliopo kibiashara kwa sasa kitaifa na kimataifa kinachotakiwa kwa watanzania kuiongeza ubora wa bidhaa, huduma na muonekano unaovutia kuanzia kwenye bidhaa husika, vifungashio, mikebe kwa lengo la kuongeza thamani na iwe rahisi kutambulika na kuvuta wanunuzi.
Pia amefafanua kwamba ili kuhakikisha watanzania wanafanya vizuri BRELA, imejipanga kuendelea kutoa elimu kwa wajasiriamali na wabunifu ili waweze kufanya bunifu zitakazowawezeshak utambulika kirahisi sokoni na kuhimili ushindani.
Kwa upande wake, Mhadhiri wa UDSM, Dkt Perfect Melkiori, amesema kuwa changamoto kubwa ambayo imejitokeza kwa wanafunzi katika chuo hicho ni wengi wa wanafunzi na wafanyakazi, kutojua thamani ya bunifu zao jambo linalofanya kurubiniwa na baadhi ya kampuni na mashirika ili kuuza bunifu zao kwa bei ndogo.
Naye, Mustafa Haji, ambaye katika kikao hicho alimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa BPRA, Khamis Juma Khamis, amelitoa rai kuwa vikao kama hivyo ni vema pia kikafanyika Zanzibar kwa lengo la kuendelea kushirikiana kwa maslahi ya taifa kwa ujumla.
Dkt Melkiori ambaye pia ni Meneja wa Miliki Bunifu wa chuo hicho, amesema kutokana na kuwepo kwa changamoto hiyo kwa wanafunzi na wafanyakazi, kwa sasa wanaendelea kutoa elimu ili kuhakikisha kundi hilo halipotezi haki ya kwa kuuza bunifu kwa gaharama ndogo kutokana na kurubuniwa na kampuni na mashirika.
0 Comments