Header Ads Widget

ACT WAZALENDO WAKEMEA SERIKALI KUFANYA BIASHARA

MWENYEKITI wa Chama cha Act Wazalendo Othman Masoud Othman amesema Serikali sio biashara na nchi haiwezi kupata maendeleo kama itaongozwa kwa msingi ya biashara.


Othman aliyasema  hayo wakati akifungua kongamano la Ngome ya Vijana ya chama hicho ambalo limefanyika katika ukumbi wa Jimbo la Ziwani Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba.


Alisema Serikali haipaswI kufanya biashara badala yake inapaswa kusimamia sera na mipango kwa manufaa ya maendeleo ya Wananchi wake na iwapo Serikali ikifanya biashara itafika pahala nchi haiwezi kutawalika.


Othman ambae pia Makamu wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwanataalum Mkongwe wa Sheria alisema kama Serikali inataka kufanya biashara inapaswa kukata leseni badala ya kufanya biashara nyuma ya mgongo wa Serikali.


Aidha Othmani Masoud amesema suala la uwazi katika matumizi ya fedha za umma lina umuhimu mkubwa katika kujenga msingi ya utawala bora.


Alisema ili Zanzibar ipige hatua za maendeleo kwa haraka ni lazima tuanzishe sheria zinazomheshimu Mwananchi kwa sababu Mwananchi ndio mfalme mbele ya Serikali.


Akizungumzia Msingi ya Demokrasia na Utawala Bora alisema Viongozi wa Vyama vya Siasa na wanachama wanapaswa kuheshimu katiba na sheria za nchi hasa wanapozungumzia masuala ya Demokrasia kupitia uchaguzi.


Alisema baada ya mapinduzi mwaka 1964 nchi ilikuwa inaendeshwa kwa kutumia sheria zilizokuwa zikitungwa na kutekelezwa na baraza la Mapinduzi (DEGREES) kabala ya Rais wa Awamu ya Pili Marehemu Aboud Jumbe Mwinyi kuamua mwaka 1979 Zanzibar kuandika Katiba yake ili kuimarisha msingi ya Demokrasia na Utawala Bora.


“leo anapotokea Mjinga Mmjoa anasema hatutoi nchi kwa kikaratasi maana yake aliekuwepo ndio anatakuwepo tutarithishana sisi kwa sisi, Muulize anatokea nchi gani, wewe unatetea mapinduzi gani baada ya mapinduzi nchi iliendeshwa kwa Degree na mwaka 1979 nchi iliamua kutunga katiba,”


Alisema kwa mujibu wa katiba yam waka 1984 imesema Mapinduzi ya Zanzibar yataendelezwa kwa kutumia utaratibu uliolezwa kwa kwenye katiba ambapo msingi mmoja ni watu wana haki ya kuchagua na kuchaguliwa.



Naye Naibu Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo Zanzibar, Omar Ali Shehe, akifunga Kongamano hilo amesema, Chama hicho kina wajibu wa kuitumia rika ya vijana, hasa wale ambao wamepata mwamko na  kutamani kuleta mabadiliko ya kweli, kupitia Miongozo,  Elimu, na Msimamo thabiti wa  kupigania haki zao, pamoja na kuyafikia malengo ya kutetea Mamlaka Kamili ya Zanzibar.


Mikutano ya Chama cha Act Wazalendo imeibua mijada mikubwa ya Wananchi katika Visiwa vya Unguja na Pemba baada ya kutumia muda mwingi kufichua tuhuma za ubadhirifu katika baadhi ya miradi hasa ujenzi wa majengo na miondombinu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI