Header Ads Widget

ZAIDI YA BILIONI 6 ZINATARAJIWA KUTUMIKA KATIKA TAMASHA LA KIZIMKAZI





ZAIDI ya Bilioni 6 zinatarajiwa kutumika kwa ajili ya miradi mbalimbali  ya maendeleo  katika Tamasha la asili la watu wa Kizimkazi mwaka 2024 ukilinganisha na Bilioni 02  mwaka jana.

Akizungumza na waandishi wa habari leo katika hafla ya kutambulisha wadhamini wakuu wa Tamasha hilo, Makamu Mwenyekiti wa Tamasha Mustafa Mohammed haji amesema ongezeko hilo limetokana na muamko mkubwa wa wadhamini.

Amesema Wadhamini wamejitokeza na kupelekea kuongezeka kwa Idadi ya miradi pamoja na thamani ya Tamasha hilo.

"Mwaka huu Tamasha ni tofauti na miaka iliyopita kwa wingi wa Wadhamini, Miradi ya maendeleo  pamoja na namna ya uendeshaji wa Tamasha," amesema.

Aidha Makamu Mwenyekiti amesema kuwa viongozi mbalimbali akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt Samia Suluhu Hassan na Dkt.hussein Ali Mwinyi wanatarajiwa kuzindua na kuweks mawe ya msingi  katika miradi mbalimbali ya maendeleo.

Mapema katika hafla hiyo Kamati ya Maandalizi imemtambulisha Dotto Abdallah alimaafu Dotto Magari kuwa Mhamasishaji wa Tamsha la Kizimkazi kwa mwaka 2024 ambapo amesema amejipanga kutangaza hilo kila pande ya Tanzania.

Tamasha la Kizimkazi linatarajiwa kufanyika kwa siku saba, kuanzia Agosti 18 hadi 25 huku kila siku moja ya Tamasha ikiwa na wadhamini wake.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI