Header Ads Widget

NAIBU WAZIRI SANGU APIGA MARUFUKU KUYATUMIA MAKUNDI HAYA KUFANYA KAZI ZA TASAF

 


Na Hamida Ramadhan Matukio Daima App Dodoma


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Mbunge wa Jimbo la Kwela, Mhe. Deus Sangu amepiga marufuku Walengwa wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii  (TASAF) wakiwemo  wazee wenye umri wa zaidi ya miaka 65, wenye ulemavu, akina mama wajawazito pamoja  na  watoto kufanya kazi za kujitolea   huku akionya Watendaji watakaozembea kusimamia suala hilo hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yao


Sangu  ametoa kauli hiyo  kwa nyakati tofauti wakati akizungumza na Wananchi  wa Kata ya Lusaka  kwenye mikutano ya hadhara iliyofanyika  kwenye  vijiji vya Lowe, Lusaka, Kizumbi na Kamnyazya  vilivyopo Jimbo la Kwela , Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga  Mkoani  Rukwa, Ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo.

 


Amezitaja kazi hizo za kujitolea ambazo huratibiwa na TASAF kuwa ni ulimaji wa  barabara pamoja na   uchimbuaji wa  mitalo ya barabara


Amesema kundi hilo lisisumbuliwe kufanya kazi hizo kwani  sio sawa kutokana na hali zao. 


Katika hatua nyingine Sangu amezitaka Kaya zinazonufaika na Mpango wa TASAF kuhakikisha kama zina  wanafunzi waliohitimu kidato cha sita na wanatarajia kujiunga Chuo Kikuu wawasilishe majina yao  katika Ofisi za  Halmashauri zao ili waweze kupata kipaumbele cha kupata  mkopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu utakaowawezesha kuendelea na masomo ya Chuo Kikuu kwani Bodi  hiyo imeingia mkataba na TASAF 



Amesema lengo la TASAF kuingia mkataba na Bodi ya Mikopo wa Elimu ya Juu ni kuhakikisha  watoto wanaotoka katika Kaya maskini hawakosi mkopo ili kuhakikisha  wanafaulu  ili badae waweze kurudi kwa ajili ya kuzikomboa Kaya zao kwenye lindi la umaskini.


Amesema ni jambo lisilokubalika chini ya Uongozi makini wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuona Mtoto aliyetoka kwenye kaya maskini kasoma  na wazazi wake ni wanufaika wa TASAF lakini anakosa mkopo anapotaka kujiunga Chuo Kikuu



Kufuatia hatua hiyo Mhe.Sangu  amewaagiza Waratibu wa TASAF wa  Mikoa pamoja na Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri zote nchini kuhakikisha wana wasaidia  watoto hao ili waweze kutimiza ndoto zao 



Aidha, Mhe.Sangu amezitaka Kaya zenye  watoto ambao ni Walengwa wa Mpango wa TASAF lakini Watoto hao hawajabahatika kujiunga kidato cha kwanza  wachangamkie fursa ya ufadhili wa masomo unatolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu kujiungana. 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI