Header Ads Widget

MIKOPO ASILIMIA 10 KWA VIJANA SIO ZAWADI REJESHENI -DR TUMAIN MSOWOYA

TAZAMA VIDEO BOFYA LINK HII

Dr.Tumaini Msowoya Mjumbe wa  kamati ya siasa ya  CCM Mkoa wa Iringa , akizungumza na Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM Wilaya ya Mufindi katika kongamano la Vijana.

Na Fredrick Siwale -Matukio Daima APP Mufindi.  

RAI hiyo imetolewa Wilayani Mufindi mkoani Iringa na Mjumbe wa kamati ya siasa ya  CCM Mkoa wa Iringa Dr.Tumaini Msowoya,wakati wa kongamano la Vijana UVCCM Wilaya ya Mufindi kwa niaba ya Ndg.Leonard Mahende Qwihaya mgeni rasmi Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa.

Dr.Msowoya alisema mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Serikali kupitia Halmashauri za Wilaya Nchini sio zawadi wala sadaka bali inapokopwa irejeshwe ili kutoa fursa kwa wengi kukopa na kuendelea kujiinua kiuchumi  na Kimaendeleo .                            


"Zipo taarifa kuwa Vijana mkikopa mnasumbua kurejesha na kuipa ugumu Serikali katika ufuatiliaji wa mikopo hiyo na ninyi kuonekana ni sehemu ya Watu wakolofi " .Alisema Dr. Msowoya.


Vile vile aliwataka Vijana kuunga mkono shughuli za Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa na Dr.Samia Suluhu Hassan, Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Halmashauri za Wilaya na si vinginevyo .


Aidha alisema Vijana waache uoga wakati ikifika wa kuboresha Daftari la kudumu la Mpiga kura kujitokeza ni wajibu na ikipendeza kuwania nafasi ni haki ila kufanya fitina ni sawa na kupigana shoti ya umeme wenyewe kwa wenyewe.                                


" Tusipigane shoti na tuliokopa turejeshe ili kuleta sifa nzuri kwa Vijana wa Chama cha Mapinduzi." 


Alisema haiwezekani Serikali kutoa fedha za kutekeleza miradi na mikopo kwa Vijana, Wazee na Wanawake halafu Vijana muonekane kuwa ni chanzo cha changamoto hiyo.                                         


Mwenyekiti UVCCM Wilaya ya Mufindi Ndg.Christian Mahenge  ,alimhakikishia Mgeni rasmi Dr.Msowoya kuwa Vijana wapo tayari kutekeleza sera za CCM kwa vitendo na kuenzi kazi nzuri inayofanywa na Dr.Samia Suluhu Hassan kwani zinajieleza na kuonekana.                      


Ndg.Mahenge alisema hakuna ubishi kuwa kazi zinazofanyika zinaonekana na hasa katika miradi ya Maendeleo ya Elimu,Afya ,Maji na miundo mbinu .                     


" Vijana Mufindi tumejipanga kuhakikisha tunashiriki vizuri kwenye Chaguzi zote kuanzia Serikali za Mitaa,Daftari la kudumu la Mpiga kura na hadi Uchaguzi Mkuu wa mwakani 2025 na kwamba " Mufindi  wanazima zote wanawasha kijana"             


Ndg.Mahenge alikabidhi cheti cha pongezi na shukuran kwa mgeni rasmi Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Ndg.Qiwihaya kuonyesha kuwa Vijana wanatambua Mchango wake kwao.


Upande wake  Aizack Mbuya ,Katibu UVCCM Wilaya ya Mufindi  alipongeza kwa dhati Viongozi  wa  CCM  kuanzia ngazi ya Matawi , Kata, Wilaya , Mkoa hadi Taifa .                     


Aidha Wasanii Wilaya ya Mufindi walikabidhi tuzo zao kwa mgeni rasmi na kuziomba Mamlaka zitoe fursa kwa Chama cha Wasanii kutumia baadhi ya maeneo kutengenezea maudhui ya sinema zao.


Chama cha Wanii na Waigizaji Wilaya ya Mufindi TDFA mwaka Jana kwa Mkoa wa Iringa kulikuwa na tuzo 12 na Mufindi ilichukua 9 na mwaka huu 2024 kulikuwa na tuzo 16 na Mufindi inejichukulia tuzo 14


"Haya ni Maendeleo tunaomba Jamii izikubali kazi zetu na tupewe Ushirikiano kwa vitendo".       

Dr.Msowoya akipokea cheti cha heshima  kutoka kwa Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Mufindi kwa niaba ya Mgeni rasmi wa kongamano hilo Ndg.Leonard Mahende Qwihaya Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa .
Ndg.Christian Mahenge - Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana UVCCM Wilaya ya Mufindi akitoa neo kwa Vijana .


Post a Comment

1 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI