Na Hamida Ramadhan Matukio Daima app Dodoma
JUMLA ya vijana 3,000 kutoka katika maeneo mbalimbali Tanzania Bara na Zanzibar wataadhimisha Siku ya Vijana ya Kimataifa kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo ya vijana
NAIBU Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Akira na wenye Ulemavu Patrobas Katambi amesema Lengo kuu la kuadhimisha Siku ya Vijana ya Kimataifa ni kuiwezesha Jumuiya ya Kimataifa na jamii kwa ujumla kupata fursa ya pamoja ya kusherehekea na kutambua nafasi na mchango wa vijana katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwenye nchi zao, tanzania tukiwemo.
Waziri huyo amesema Kupitia kongamano hilo, vijana watajadili masuala mbalimbali ikiwemo; kutoa maoni kuhusu Dira ya Taifa ya Maendeleo (Tanzania tuitakayo 2050), vijana na matumizi ya fursa za kidijitali, vijana na uchumi, afya ya akili, na saikolojia ya vijana.
" Kabala ya maadhimisho hayo shughuli zitakazotekelewa ni pamoja na Agosti 10 na 11, 2024 kutakuwa na kongamano la vijana litakalofanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete, Jijini Dodoma.
Na kuogeza "Agosti 12, 2024, itakuwa ni siku ya kilele cha kuadhimisha Siku ya Vijana Kimataifa, ambapo vijana na wadau mbalimbali wa maendeleo ya vijana watashiriki. Mgeni rasmi wa maadimisho ya mwaka huu anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), " Ameeleza
Amebanisha kuwa, Kilele cha maadhimisho hayo kitaambatana na uzinduzi wa Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana ya mwaka 2007, toleo la mwaka 2024. Sera hii pamoja na mkakati wa utekelezaji wake ni nyenzo muhimu kwa wadau wa maendeleo ya vijana nchini.
Itambulike kwamba, vijana ndio kundi kubwa, kwa mujibu wa takwimu za Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, idadi ya vijana wenye umri wa kuanzia miaka 15-35 ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni 21,312,411 sawa na (34.5%) ambapo kwa Tanzania bara ni 20,612,566 sawa na (34.4%).
"Kwa kutambua kuwa vijana ndio nguvu ya kufanya kazi, wabunifu na chachu ya mabadiliko katika jamii yoyote ile. Pia Vijana ndiyo warithi wa historia katika Mataifa yao. Kwa mantiki hii hatuna budi kutambua na kuthamini mchango wa vijana katika maendeleo ya nchi yetu, " Amesema Katambi.
Na kuongeza "Kwa mwaka huu 2024, tarehe 12 Agosti, nchi yetu itaungana na nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa kuadhimisha Siku ya Vijana ya kimataifa.
Amesema Maadhimisho hayo yatafanyika Mkoani Dodoma, chini ya kauli mbiu “Vijana na matumizi ya fursa za kidijitali kwa maendeleo Endelevu”. Kauli mbiu hii inazisisitiza jumuiya za kimataifa kuwekeza kwa vijana kwa kuwaunganisha na fursa za kidijitali kwa sababu ulimwengu wa sasa umetawaliwa na matumizi ya teknolojia ya kidijitali kama vile; matumizi ya simu, pamoja na uvumbuzi unaotokana na akili mnemba (Artificial inteligency).
" Kwa kuzingatia matumizi ya fursa za kidijitali kwa maendeleo endelevu, tutakubaliana kuwa dhana ya vijana kupatiwa ujuzi wa kidijitali ni muhimu sana kwa kizazi cha sasa na vizazi vijavyo, ili viweze kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwenye nchi yetu, " Amesema.
Maadhimisho hayo pia yataambatana na shughuli za maonesho ya shughuli za kibunifu za vijana katika viwanja vya nje vya ukumbi wa Jakaya Kikwete Dodoma. Pia wadau watapata fursa ya kuonesha kazi zao na kutoa huduma mbalimbali kwa vijana kama vile; upimaji wa afya kwa hiari, ushauri nasihi, elimu ya afya ya uzazi pamoja.
Mwisho
0 Comments