Mwanamke anayefahamika kwa jina la Rehema Maulid (30) mkazi wa eneo la Wawaso wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha, amefariki dunia kwa madai kuwa ni baada ya kupigwa na kitu kizito kichwani na mchepuko wake kwa tuhuma za kuiba laki nne na nusu wakiwa kwenye chumba cha kulala wageni maarufu kama Gesti wilayani humo.
Jeshi la polisi mkoa wa Arusha limethibitisha kuwepo kwa tukio hilo, na limesema tayari mtuhumiwa wa tukio hilo ameshilikiliwa na muda wowote atafikishwa Mahakamani.
0 Comments