Header Ads Widget

AFUKIWA NA KIFUSI MRADI WA BARABARA KIGOMA

 

Mkuu wa wilaya Kigoma Salum Kali (kulia) akiongea Michael Christopher majeruhi wa tukio la kufukiwa na kifusi eneo la Rutale manispaa ya Kigoma Ujiji

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

 

MICHAEL Christopher fundi ujenzi mkazi wa mtaa wa Kirungu kata ya Machinjioni manispaa ya Kigoma Ujiji amenusurika kifo baada ya kufukiwa na kifusi cha barabara wakati akichimba mtaro kwa ajili ya ujenzi wa karavati katika mradi wa barabara ya Kilometa tisa kutoka Katonga kupitia Burega hadi Ujiji.

 

Fundi Ujenzi huyo alikumbukwa na tukio hilo jana mchana eneo la Rutale akiwa katika utekelezaji wa mradi wa barabara hiyo kupitia mradi wa TACTIC unaofadhiliwa na benki ya dunia ambapo baada ya kufikiwa na kifusi wafanyakazi wenzake waliwahi kumuokoa na Kumuwahisha hospitali ya mkoa Kigoma Maweni kwa matibabu.

 

Mkuu wa wilaya Kigoma,Salum Kali alitembelea eneo la tukio na kuzungumza na wafanyakazi na wasimamizi wa mradi huo akiwataka kuchukua tahadhari ili madhara yasiweze kutokea kwa watu wanaoshiriki kwenye mradi huo.

 

Sambamba na hilo Mkuu huyo wa wilaya alitembelea nyumbani kwa majeruhi huyo Mtaa wa Kirugu kata ya Machinjioni manispaa ya Kigoma Ujiji ambapo alienda kumpa pole na kumjulia hali sambamba na kumpa msaada kwa ajili ya matumizi yake na familia kwa muda wote atakaokuwa nyumbani akipata matibabu. 

 

Akizungumza mbele ya Mkuu wa wilaya aliyemtembelea nyumbani Fundi ujenzi huyo, Michael Christopher alimshukuru Mkuu wa wilaya kwa hatua hiyo ya kumtembelea na kumfariji kwani imemtoa moyo kuona serikali iko Pamoja naye.

 

Christopher alisema kuwa baada ya kuangukiwa na kifusi na kuokolewa na wenzake alikimbizwa hospitali ya rufaa ya mkoa Kigoma Maweni ambapo alifanyiwa vipimo na kwa sasa anaendelea vizuri.

 


Eneo la Rutale ambapo kulitokea ajali hiyo ya mtu kufukiwa na kifusi


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI