Na Fredrick Siwale -Matukio Daima APP Mufindi.
MJUMBE wa kamati ya siasa ya Chama Cha mapinduzi (CCM ) mkoa wa Iringa Dickison Mwipopo amewataka UVCCM wilaya ya Mufindi kujiepusha kutumiwa kwa maslahi ya Wachache bali wasimame imara na kuitetea katiba ya CCM na Watendaji kutambua wajibu wao ndani ya Chama .
Mwipopo alitoa kauli hiyo wakati wa kikao Cha Baraza la umoja wa Vijana wa Chama Cha mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Mufindi mkoani Iringa .
Alisema Vijana wananafasi kubwa ya kukijenga Chama hicho iwapo hawatakubali kutumika kwa maslahi ya wachache.
Katika baraza hilo limewatunuku vyeti Viongozi mbali mbali ,wakiwemo Waheshimiwa Wabunge wa Majimbo yote matatu ya Uchaguzi,Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Dr.Linda Salekwa na Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya ya Mufindi na Halmashauri ya Mji Mafinga ,kwa Mchango wao mkubwa kujenga CCM na kuimarisha Jumuiya hiyo UVCCM Wilaya.
Hata hivyo UVCCM Wilaya ya Mufindi imesema UVCCM haina mbeleko ya kuwabeba wasio bebeka.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM Wilaya ya Mufindi Ndugu Christian Mahenge wakati wa kikao cha kawaida cha Baraza la Jumuiya hiyo.
Ndugu Mahenge alisema UVCCM Mufindi imejipanga na imejidhatiti kikamilifu kuhakikisha kuwa Wanashiriki kwa uadilifu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu 2024 pamoja na Uchaguzi Mkuu wa mwakani 2025.
Kikao hicho cha Baraza la Vijana UVCCM Wilaya kilifanyika kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi (Bomani) huku mgeni Mjumbe wa kamati ya Halmashauri kuu ya CCM Mkoa wa Iringa Ndugu Dickison Mwipopo.
"Nasema Vijana tumejipanga kuhakikisha kuwa CCM inapata ushindi wa kishindo katika Chaguzi zote " Alisema Ndugu Mahenge
Alisema UVCCM itapiga kura na kuchagua Viongozi ambao ni chaguo la Wananchi na sio chaguo la Viongozi Alisema Ndugu Mahenge .
CCM MUFINDI kupitia UVCCM Wilaya hakuna Kiongozi yeyote aliyopo Madarakani na Mtia nia ambaye atadhani Kuna mbeleko ya kuwabebea bali Wanachama wote wataamua nani chaguo lao.
"Sisi UVCCM Wilaya ya Mufindi tunaomba tuwahimize Vijana wenye sifa kugombea nafasi mbali mbali kwa ninyi ndio nguvu kazi na Taifa linatutegemea" Alisema Ndugu Mahenge.
Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mufindi kupitia UVCCM imeahidi kuendelea kupeperusha bendera ya ushindi wa kishindo na Kauli mbiu yake ya " Tunazima zote tunawasha kijani "







0 Comments