Header Ads Widget

"WANACHUO KUOA NA KUOLEWA SIO MTAJI". TAWETE




Na Fredrick Siwale -Matukio Daima APP Mufindi.     


WAHITIMU Wa Vyuo vya kati Nchini wameambiwa kuwa kuoa na kuolewa sio mtaji wala sio dili ,bali wajiendeleze na masomo ya juu zaidi.


Hayo yamesemwa na Muuguzi Mkuu Mkoa wa Iringa,Ndugu Moses Tawete ,wakati wa mahali ya 9 ya Chuo cha Uuguzi na Ukunga Ufamasia na Ustawi wa Jamii cha New Mafinga health and Allied Institute (NEMA HAI) .                           


Ndugu Tawete alisema imezuka tabia kwa baadhi ya Wauguzi na Wakunga kuamua  kuoa au kuolewa baada ya kuhitimu mafunzo ngazi za chini.


" Acheni kudanganyika someni hadi PhD badala ya kuitelekeza elimu ambayo Wazazi walihangaika kuwatafutia nafasi". Alisema Tawete.


Alisema Vyuo vipo nafasi zipo Wananchi changamkieno fursa hizo ili siku za usoni zije kuwasaidia badala ya elimu yenu kwenda kuoa au kuolewa.    


Jamii ya Watanzania inakatishwa tamaa na ndoto za Wazazi ambao lengo lao ni kuona Watoto wao wanasonga mbele.



"Wahitimu Jamii inawategemea katika kada hii ya Uuguzi na Ukunga, Ufamasia na Ustawi wa Jamii si kwa bahati mbaya hivyo msiishie hapa kajiendelezeni badala ya kujiona sawa na wasioelewa" Alisema Ndugu Tawete.


Alisema inasikitisha sana kuona Sekta inayotegemewa ila wanaotegemewa ni kama nao hawajitambui  badala ya kusoma wanaamua kuoa na kuolewa nakusahau elimu nyuma.


Pamoja na kukipongeza Chuo cha NEMA HAI kuendelea kufanya vizuri aliwaomba Wahitimu kuzingatia taratibu, kanuni na miiko ya Uuguzi na Ukunga kwa kuishi maisha halisi ya Ukunga.


"Sitegemei kuja kusikia eti kuna Mhitimu badala ya kuendelea na masomo ngazi za Juu anakimbilia kuolewa au kwenda kuwa mpiga lamli " Alisema Ndugu Tawete.


Katika tasnia ya Uuguzi na Ukunga kwa Wafamasia na Ustawi wa Jamii Wahitimu wetakiwa kuacha kwenda kutamani maisha makubwa nje ya kibato cha halali.

Bw.Bakari Maulid Sesanyi - Mkuu wa chuo cha NEMA HAI.


Awali Mkuu wa chuo Cha NEMA HAI Bw.Bakari Maulid Sesanyi akisoma risala mbele ya Mgeni rasmi Muuguzi Mkuu Mkoa wa Iringa Ndugu Moses Tawete alisema Chuo hizo kilianzishwa mwaka rasmi January 2012 kwa malengo mtambuka.


Bw.Sasenyi alisema  malengo ilikuwa ni kuwawezesha Wanafunzi ambao hawakupata nafasi ya kuendelea na kidato cha kwanza baada ya kuhitimu elimu ya Msingi na wale walioshindwa kwenda A- level .


Walengwa wengine ni wale waliohitimu kidato cha nne kuwapatia  stadi za kazi ili wajitafutie ajira au Wajiajiri wao wenyewe chini ya Uongozi na umiliki wa familia ya Mzee Jarufu Ally Makoti (Marehemu) .

Madam Veronica Mwalusamba - Mkurugenzi wa Chuo cha NEMA HAI.


Mkuu wa chuo cha NEMA HAI Bw.Sesanyi alisema Makoti alikuwa Mkurugenzi wa kwanza wa New Mafinga health Institute mwaka 2012 ikiwa chini ya Usimamizi Msalaba Mwekundu   (TANZANIA RED CROSS SOCIETY) kwa lengo la kutoa huduma ya kwenda.


Mwaka 2014 chuo kilipewa usajili wa muda hadi mwaka 2016 ambapo kilipewa usajili wa kudumu na kupewa namba ya usajili REG /HAS/145 ambapo hadi sasa Chuo kina Jumla ya Wanafunzi 295  ,Wasichana wakiwa 202 na Wavulana 93 wanaosoma Kozi tatu katika  fani za Uuguzi na Ukunga , Ufamasia na Ustawi wa Jamii.


Upande wake Mkurugenzi wa Chuo cha NEMA HAI,Madam Veronica  Mwalusamba alisema inaishukuru Jamii ya Watanzania wanaosomesha Watoto wao katika Chuo hicho kwani wao ndio sehemu na rafiki wa karibu zaidi.


Madam Veronica Mwalusamba alisema elimu ni mtaji na kuwaomba Wazazi kushika sana elimu ili kuwarithisha Watoto elimu kwa faida ya baadaye.  


Akisoma risala mbele ya Mgeni rasmi Mhitimu Marieta Haji Willamu ,alisema Chuo kimefanikiwa kuwa na ufauru wa Viwango vya juu katika mitihani ya ndani na nje ya chuo.


Chuo kina maktaba yenye Vitabu pamoja kompyua kwa ajili ya kujjsomea ili kuongeza maarifa katika katika kada mbali mbali 



Mhitimu Marieta alisema Chuo kimeboresha Mazingira kwa ajili ya Wanafunzi kuweza kujisomea kwani Maji yapo ya kutosha ,chumba cha kompyuta ,kuwa na vyanzo na pampu mbili, visima vitatu ,na matenki mawili makubwa kwa ajili ya kuhifadhia maji.    


Katika risala hiyo Marieta alisema kila penye mafanikio hapakosi changamoto kwani katika Chuo hicho Kuna uhaba wa Vitabu vya kada ya Ustawi wa Jamii,famasia na vifaa vya kemikali za maabara kwa ajili ya mafunzo ya vitendo na kutokuwepo kwa uzio wa chuo kwa kuimarisha Ulinzi na Usalama wa Wanafunzi na mali zao . 






Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI