Header Ads Widget

ACT WAZALENDO WAIANGUKIA SERIKALI, DC KALIUA NA AFISA HABARI TAWA WATOA TAMKO


Na Matukio Daima App

Chama Cha ACT -Wazalendo kimeiomba Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kuunda kamati ya uchunguzi kupitia maeneo yote yenye migogoro ya ardhi kati ya vijiji na mamlaka ya hifadhi ili kupata suluhu la kudumu.

Rai hiyo imetolewa na Waziri kivuli WA Katiba na Sheria kutoka Chama Cha ACT -Wazalendo Maharagande Mbalali wakati alipokua akizungumza na waandishi jijini Dar es salaam amesema Kuna operesheni ya kuwaondoa wananchi hao ilianza kufanyika Agosti 2021
.
Amesema kuwa, operesheni hiyo inagusa vijiji 11 vya Usinge, Luganjo, Wachawaseme, Igagala Na.3, Igagala Na.4, Igagala Na 7, Igagala Na 9, Kombe, Tuombe Mungu na Limbu la Siasa, ambapo imesababisha madhara na kufanya uharibifu mkubwa Kwa Kaya 7,000 hadi 8,000 ziliondolewa kwenye ardhi zao na kuachwa bila makaz.

"Huu ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu kwani matendo yanayotokea huko ni pamoja na vifo vya watu 12 ambapo wengine waliuliwa kwa risasi za moto, kunyang’anywa mali zao (mifugo na mazao), vipigo, kujeruhiwa, kutozwa faini zisizo za haki, kubabimbikiwa kesi, visa kadhaa vya ubakaji na wengine wamekimbia vijiji hivyo"amesema Waziri Kivuli Maharagande.

Amefafanua kuwa, chanzo cha mgogoro wa ISAWIMA umetokana na Serikali kupitia TAWA, TFS na Mkuu wa Wilaya ya Kaliua kutwaa eneo la hifadhi ya ardhi ya vijiji 11 na kubadilisha kuwa Pori la Akiba la Igombe bila ridhaa yao, mwaka 2007 ambapo vijiji 11 vilikubaliana kutenga sehemu za ardhi zao za vijiji eneo lenye ukubwa wa kilomita za mraba 1,800 kwa ajili ya kuanzisha jumuiya ya hifadhi ya wanyama pori iliyojulikana kwa jina la ISAWIMA (Igombe and Sagara Wildlife Management Area).
 
Kati ya 2016 na 2021, kutokana na uhaba wa ardhi na ongezeka la watu wanavijiji walifikia makubaliano ya kupunguza ukubwa wa eneo lao la hifadhi hadi Kilomita za Mraba 1,300 nakuacha kilomita za mraba 500 kwa matumizi ya ardhi ya vijiji, lakini, Serikali ilichukua kilomita 1300 na kuanzisha pori la Akiba la Igombe na kuacha kilomita 500 kwa Tangazo la Serikali (GN) Na. 455 la mwaka 2021.

Aidha, kutokana na kadhia hiyo, Act wanaiomba Serikali kusitisha zoezi la operesheni ya kuwaondoa wananchi hao kwenye ardhi yao na kuachilia mifugo waliyoishikia bila masharti yoyote, sambamba na kulitaka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuunda kamati ya uchunguzi wa
matukio hayo.

"Tunarudia wito kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuunda kamati ya kupitia maeneo yote yenye migogoro ya mipaka kati ya vijiji na mamlaka za hifadhi nchini, tunataka hatua zichukuliwe kwa watendaji, maafisa na watumishi wa mamlaka
wanaofanya vitendo vya uvunjifu wa Haki za Binadamu ISAWIMA kuanzia 2021 hadi sasa"amesema

Ameongeza kuwa tayari wameshaandaa barua ya kupeleka malalamiko na kuiomba Tume ya haki za binadamu na Utawala bora kufanya uchuguzi wa matukio hayo ya kikatili, kama
alivyoahidi akiwa ziarani Kiongozi wa chama Mstaafu Ndg. Zitto Zuberi Kabwe, huku akiwataka walioshiriki katika tukio hilo kuchukuliwa hatua za kisheria.

Kutokana na taarifa iliyotolewa na Chama Cha ACT -Wazalendo inayodai kutokea kwa juu matukio hayo, Mtandao wa Matukio Daima umefanya jitihada za kuzungumza na Mkuu wa Wilaya ya Kaliua na Afisa habari wa TAWA wamekanusha taarifa hizo na kudai hawajapokea malalamiko yoyote kutoka kwa wananchi wa vijiji hivo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI