Mbunge wa Jimbo la Lupa ,Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya Masache Njelu Kasaka ameibana Serikali iangalie namna ya kukokotoa upya bei ya umeme baada ya mradi wa kufua nishati hiyo wa Julius Nyerere (JNHPP)kukamilika ili kupunguza gharama kwa wananchi.
Kasaka akiuliza swali bungeni amehoji "Serikali haioni haja ya kupitia upya ukokotoaji wa bei za unit na baadaye kushusha bei ili kuleta nafuu kwa mtanzania "
Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga amesema, gharama za umeme si za uzalishaji pekee bali zinahusisha usambazaji na usafirishaji na uwekezaji.
Pia Kasaka ameisihi serikali kufanya jitihada za haraka kusambaza umeme maeneo ya uchimbaji wa dhahabu (migodini ) Ili kurahisisha uzalishaji kwa njia za kisasa.
0 Comments