MWILI wa aliyekuwa Mjumbe wa baraza la Wawakilishi viti maalum mkoa wa Kaskazini Unguja, Panya Ali Abdalla aliyefariki akipatiwa matibabu nchini India, unatarajiwa kukabidhiwa kwa ndugu zake leo Jumamosi.
Mjumbe huyo aliyefariki usiku wa kuamkia jana nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu baada ya kuugua kwa muda mrefu ambapo kabla alipatiwa matibabu katika hospitali za ndani.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera, Utaratibu na Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Hamza Hasan Juma amesema serikali kwa kushirikiana na familia imeendelea kuratibu mipango ya mazishi na kurudisha mwili wa marehemu kisiwani hapa.
"Kwa upande wetu serikali tumekamilisha mipango ya kusafirisha mwili na watu ambao walimuuguza ambapo tunarajia mwili huo utapokewa siku ya Jumamosi mchana na watakabidhiwa familia yake," amesema Hamnza
Pia, amesema Mwakilishi huyo alikuwa mahiri na alifanikisha kwa kiasi kikubwa utekelezaji wa mipango ya serikali.
0 Comments