Mjumbe wa kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) mkoa wa Iringa Dickson Mwipopo amechangia kiasi Cha Tsh milioni 2 Kwa ajili ya ujenzi wa Nyumba ya katibu wa Jumuiya ya wazazi wilaya ya Iringa Vijijini huku akiahidi Kuchangia Vifaa vya TEHAMA Kwa ajili ya ofisi.
Mwipopo ambae alikuwa Mgeni Rasmi ametoa msaada huo leo wakati wa kikao Cha Baraza kuu la jumuiya ya wazazi wilaya ya Iringa Vijijini lililofanyika ukumbi wa Siasa ni Kilimo mjini Iringa .
Alisema kuwa ujenzi wa Nyumba ya katibu ni jambo la msingi pia Vifaa vya TEHAMA katika ofisi ya jumuiya ya wazazi wilaya ya Iringa Vijijini ni muhimu sana na hivyo atahakikisha anafanikisha Vifaa hivyo kama Kompyuta na Printa Kwa ajili ya ofisi .
Pia Mwipopo amejitolea kununua simu Kwa ajili ya Vijana watakaofanya kazi ya usajili wa wanachama kidigitali katika jumuiya hiyo .
Katika hatua nyingine Mwipopo amewataka wazazi kuendelea kumsemea vizuri Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoofanya na kuwa Dkt Samia amekuwa kiongozi wa mfano katika kutekeleza miradi mikubwa ya kimaendeleo kwa watanzania .
Hivyo kupitia miradi hiyo ni vema Kila mmoja kuendelea kuisemea miradi hiyo pia kuendelea kumpongeza Mheshimiwa Rais kwa kazi nzuri.
TUKIO ZIMA TAZAMA KUPITIA KIPINDI MAALUMU KITAKACHOKUJIA HIVI PUNDE CHANEL YA MATUKIO DAIMA TV
0 Comments