Header Ads Widget

WAZEE MUFINDI WATUNZWE NA KULINDWA NI TUNU.

 


Wazee wakiwa katika picha ya pamoja Viongozi wa Wilaya ya Mufindi na Kata ya Boma baada ya kumaliza kikao.

Na Fredrick Siwale -Matukio Daima APP Mufindi.


JAMII Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa ,imetakiwa  kuwalinda na kuwatunza Wazee ambao ndio tunu iliyopo kwa Kizazi hiki cha sasa.                                 

Wito huo umetolewa katika mkutano wa CCM Wilaya na Katibu Siasa na Uenezi Wilaya Bw.Dickison Nathan Lutevele (Villa) wakati akizungumza na Wazee wa Mufindi.                               


Bw.Villa alisema Wazee ni tunu na wanastahili kutunzwa , kupendwa na kuheshimiwa na Watu wote pasipo kubaguliwa ,kutengwa wala kunyanyasika.              


"Wazee wangu nimewaita ili kuzungumza naye kwa mstakaabali wa kufahamiana kuwa karibu na kushirikiana nanyi katika kusaidia kutoe elimu ya maelezi na makuzi kwa Vijana wetu na Jamii kwa ujumla." Alisema Villa.            


Alisema sasa hivi vipo viashiria vya uhalifu kwa baadhi ya maeneo hapa vinavyofanywa na Watu wasioitakia mema Nchi yetu kwa Wazee , Wanawake na Watoto ambavyo vinatakiwa kukemewa kwa nguvu zetu zote.                                


"Wazee tusaidieni kufundisha na kukemea vitendo vya uhalifu ili kizazi hiki kiendelee kuwa salama bila kujali itikadi zetu dini na Vyama vya Kisiasa .               

Gift Mwachang'a Katibu wa Siasa na Uenezi Kata ya Boma akifuatilia na kuandika baadhi ya taarifa ndani ya Ukumbi wa CCM Wilaya ya Mufindi.


Alisema Chama cha Mapinduzi (CCM) matamanio yake ni kuona amani ,upendo na utulivu uliopo hapa Nchini vinaendelea kudumu kwa maslahi mapana ya Taifa.                  


Aidha Katibu wa Siasa na Uenezi Wilaya ya Mufindi Bw.Villa aliwaomba Wazee Mufindi kuhakikisha wanatoa elimu kwa Jamii kujiandikisha na kupiga kura Uchaguzi wa Serikali za Mitaa pindi muda utakapowadia.             


Alisema zoezi la kujiandikisha na kupiga kura ni la muhimu sana kwa Wananchi hivyo kila mmoja awe barozi wa mwingine ,hasa kwa kuhamasisi kujiandikisha, kupiga kura na bila kusahau haki ya msingi ya kugombea , kuchagua na kuchaguliwa.                          


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI