WAUGUZI nchini wametakiwa kutoa huduma kwa upendo utu na uadilifu kwani wao ni kama mwanga kwa wagonjwa wanapokwenda kupata huduma.
Hayo yamesemwa mjini Kibaha na Katibu Tawala Mipango na Uratibu wa Mkoa wa Pwani Edina Kataraiya ambaye alimwakilisha Naibu Waziri wa Afya Dk Godwin Mollel wakati wa Maadhimisho siku ya Uuguzi kimkoa.
Kataraiya alisema kuwa kada ya uuguzi ni uti wa mgongo wa huduma za afya ndiyo sababu serikali inaendelea kuboresha mazingira kwani bila ya wauguzi hakuna huduma hizo hivyo watoe huduma kama kiapo chao.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA) Steven Brown amesema kuwa katika Muundo wa Utumishi wa Kada ya Uuguzi na Ukunga ambacho kinamtaka Ofisa Muuguzi kabla hajafikia Kiwango cha mwisho cha Mshahara wake yaani TGHSG awe na Masters ambacho ni kikwazo kwa wauguzi.
Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Pwani Kusirye Ukio amesema kuwa huduma wanayotoa wauguzi ni ibada na Hospitali ni madhabahu hivyo waendelee kudumisha ibada zao.
0 Comments