Header Ads Widget

VIJANA KUTOKA JIMBO LA BUKOBA VIJIJINI WANUFAIKA NA ELIMU YA USALAMA BARABARANI.

 










Na Mariam Kagenda,Kagera 

Mbunge wa viti maalumu kupitia  tiketi ya chama cha Demokrasia na maendeleo- CHADEMA- kutoka jimbo la Bukoba vijijini Bi Conchesta Rwamulaza amewakutanisha zaidi ya vijana mia nne kutoka kata  zote za Halmashauri hiyo ili wapatiwe elimu ya usalama barabarani na namna ya kuepuka kufanya vitendo vya  ukatili wa kijinsia ambapo elimu hiyo  imetolewa na maafisa kutoka jeshi la polisi wilaya ya Bukoba.


Mheshimiwa Rwamulaza amesema kuwa kutokana na changamoto  ya kuongezeka Kwa vitendo vya ukatili hususani kwa watoto ikiwemo pia ajali za barabarani ambazo wakati mwingine  zinasababishwa   na vijana hao ambao wengi wao ni boda boda ameamua kuwakutanisha  kwa pamoja bila kujali itikadi za vyama vyao  ili wapatiwe elimu ya namna ya kukabiliana na changamoto hizo.


Mbali na utolewaji wa elimu ,pia Mbunge huyo ametoa vifaa vya michezo kwa timu 11 za mpira za vijana kutoka Halmashauri ya Bukoba ikiwemo mipira 11 na jezi za michezo vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni tisa.


Kwa upande wao maafisa wa jeshi la polisi waliotoa elimu kwa vijana hao akiwemo mkuu wa dawati la jinsi wilaya ya Bukoba Bi Betrida Mbinga na coplo wa usalama barabarani Mohamed  Sadick wamemshukuru mbunge huyo Kwa kuwa na maono makubwa ya kuwakutanisha vijana hao ili wapatiwe elimu ambayo itawasaidia kujiepusha na ukatili pamoja na masuala ya ajali zinazoweza kuepukika.


Baadhi ya vijana hao wamemshukuru mbunge huyo kwa kukutanisha kundi kubwa la vijana bila kujali itikadi za vyama vyao.


Vijana hao wameweza kumpatika Mbunge huyo zawadi  ya vitu mbalimbali kama  shukrani kutoka kwa vikundi vya vijana wanaofanya shughuli za ujasiliamali kupitia vikundi kwa ufadhili wa mbunge huyo aliowapatia mtaji kwa miaka miwili iliyopita na sasa wameanza kunufaika.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI