Header Ads Widget

WATUMISHI MKALAMA WAASWA KUWA WAZALENDO,KUFANYA KAZI KWA BIDII KUWAENZI MASHUJAA

 


Na Thobias Mwanakatwe,MKALAMA 

WATUMISHI  wilayani Mkalama mkoani Singida wametakiwa kuwa wazalendo na kufanya kazi kwa bidi katika ili kuwaenzi mashujaa wa nchi waliopigana kwa ajili ya taifa la Tanzania.


Katibu Tawala Wilaya ya Mkalama, Peter Masindi, alisema hayo jana wakati wa zoezi la usafi liliofanyika katika Hosipitali ya Wilaya ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya mashujaa nchini.


Alisema serikali inaleta fedha nyingi kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo hivyo ni wajibu kwa watumishi kuwajibike pamoja katika kuhakikisha fedha hizo zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa. 


"Kila mmoja katika nafasi yake atimize wajibu wake, huwezi kuwa shujaa kama ukishindwa kutimiza wajibu wako, kwa kufanya hivi tutakuwa tumewaenzi Mashujaa wetu,” Masindi.


Aidha, Masindi amewasisitizia watumishi kuwahudumia wananchi kwa kutumia lugha nzuri pindi wanapokuwa wanatoa huduma kwa wananchi, kulinda maadili ya kazi pamoja na kudumisha amani na umoja baina yao  


"Tuache ubabe, tuache ufalme kwa kutumia ofisi zetu za serikali, bali tuwatumikie watanzania kwa lugha nzuri,"alisema.


 Katibu Tawala huyo amekumbusha watumishi kulinda maadili ya nchi yetu kwa kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia, vitendo vya ulawati na ushoga katika jamii zetu.


“Ndugu zangu Tuhakikishe maadili ya watoto wetu yanajengwa na sisi wazazi, yanajengwa na sisi jamii iliyopo leo, tuhahitaji jamii yenye utuvuli , amani kwa ajili kufikia maendeleo ya taifa letu,hakikisha mtoto anaenda shule, huo ndio ushujaa unaostahili,".

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI