Na Thobias Mwanakatwe,IRAMBA
MAAFISA Elimu Kata na maafisa Idara ya Elimu Awali na Msingi katika Halmashauri ya Wilaya Iramba mkoani Singida wametakiwa kutumia vizuri nafasi zao katika kuwasaidia walimu kutatua changamoto mbalimbali za kielimu kupitia usimamizi saidizi.
Afisa Elimu Taaluma Mkoa wa Singida, Regina Yagambe alisema hayo juzi wakati akifungua mafunzo ya Usimamizi Saidizi yanayotolewa na Serikali kupitia Programu ya Mradi wa Shule Bora.
“ Tunatamani tubadilishe ule utaratibu wa ufuatiliaji na badala yake tufanye usimamizi saidizi ambapo Maafisa Elimu Kata watafika kwenye vituo vyao vya kazi (shuleni) na kubaini changamoto ambapo hawataishia kuandika changamoto hizo kwenye 'log book' badala yake wataweza kumpa usaidizi Mwalimu Mkuu na Walimu wengine katika kutatua changamoto hizo," alisema.
Alisema changamoto za walimu zitakapokuwa zinatatuliwa kwa wakati kutawawezesha hatua kufanya vizuri hata kufanikisha malengo ya Mtaala wa Elimu Msingi.
Naye Mwalimu Nickson Mmanyi akizungumza kwa niaba ya Maafisa Elimu Kata waliohudhuria kwenye mafunzo hayo, alisema mafunzo hayo yatawasadia kwa kiasi kikubwa katika kuboresha usimamizi wa shule hususani eneo la uongozi na hivyo kuinua kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi ambao ndio walengwa.
“Tunawashukuru Shule Bora kwa mafunzo haya kwani kupitia mafunzo kwayo tunaamini yatasaidia katika kuimarisha usimamizi wetu wa mifumo ya ujifunzaji, ufundishaji, ujumuishi na usalama wa wanafunzi, alisema.
Mradi wa Shule Bora ni programu inayofadhiliwa na Shirika la Misaada la Uingereza (UK AID) kupitia Shirika lake la Maendeleo la Kimataifa (DIFD/FCDO) na inatekelezwa katika mikoa tisa nchini ambayo ni Singida, Dodoma, Katavi, Pwani, Dodoma, Rukwa,Kigoma, Mara na Tanga.
Katibu Tawala huyo amekumbusha watumishi kulinda maadili ya nchi yetu kwa kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia, vitendo vya ulawati na ushoga katika jamii zetu.
“Ndugu zangu Tuhakikishe maadili ya watoto wetu yanajengwa na sisi wazazi, yanajengwa na sisi jamii iliyopo leo, tuhahitaji jamii yenye utuvuli , amani kwa ajili kufikia maendeleo ya taifa letu,hakikisha mtoto anaenda shule, huo ndio Ushujaa unaostahili,".
0 Comments