Na Gabriel Kilamlya Matukio Daima APP NJOMBE
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Njombe ambaye ni mkuu wa wilaya Kissa Kasongwa ameagiza kukamatwa kwa wajumbe wote wa bodi ya Lupembe Saccos ndani ya saa 48 ili warejeshe fedha zaidi ya shilingi milioni 600 za wananchi zinazodaiwa kupotea.
Kasongwa ametoa agizo hilo huku akielekeza kukamatwa na kuhojiwa kwa Ofisa ushirika wa halmashauri ya wilaya ya Njombe Bwana Fredy Mwankusye ambaye anatajwa kushindwa kusimamia vyama vya ushirika.
Mrajisi msaidizi wa vyama vya ushirika mkoa wa Njombe Edmund Masawe amesema tayari baadhi ya wahusika wa Lupembe Saccos Wameshasimamishwa kazi huku timu ya ukaguzi ikitarajiwa kuwasili wakati wowote.
Naye Mbunge wa jimbo la Lupembe Edwin Swalle ametaka viongozi wote waliosimamishwa kazi wakamatwe na waanze kuhojiwa ili fedha za wananchi wa Lupembe zirejeshwe huku Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Njombe Christopher Sanga akisema lazima fedha za wananchi zirejeshwe.
Awali meneja wa Lupembe Saccos Oliver Kinyamagoha aliyesimamishwa kazi amesema kutokana na changamoto kubwa iliyojitokeza anaomba msaada wa kufanyika kwa uchunguzi.
Baadhi ya wananchi na wanachama wa Lupembe Saccos akiwemo Justin Kiwale,Rehema Malekela Malaki Kabelege na Romanus Hongoli Wanasema wamekosa imani na bodi pamoja na ushirika na hivyo wanataka fedha zao.








0 Comments