Header Ads Widget

RC BABU AIPONGEZA HALMASHAURI YA SIHA KWA KUVUKA MALENGO YA MAKUSANYO YA KODI.

 


NA WILLIUM PAUL, SIHA. 


MKUU wa mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu ameipongeza halmashauri ya wilaya ya Siha kwa kufanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato na kupelekea kuvuka lengo kuzitaka Halmashauri zingine kuiga mfano huo. 



Babu ametoa kauli hiyo leo wakati wa kikao maalum cha Baraza la Madiwani kupitia na kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30 mwaka 2023.



Alisema kuwa, halmashauri hiyo imeendelea kufanya vizuri na kupelekea kupata hati safi kwa miaka mitatu mfululizo ambapo katika kipindi hicho imepata hoja nane za CAG. 



"Nimeona kazi kubwa ambayo mmeifanya Siha na kupelekea kupunguza hoja za CAG mpaka kufikia 8 sasa nataka watumishi shirikianeni ili mwaka tusiwe na hoja hata moja ya Mkaguzi na hili linawezekana kwenu" Alisema Babu. 



Kwa upande wake,  Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Dkt. Haji Mnasi alisema kuwa halmashauri hiyo imeweza kuvuka lengo la ukusanyaji mapato kutokana na ushirikiano uliopo baina ya watumishi wa halmashauri hiyo na Madiwani. 


Mwisho..

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI