Na Matukio Daima App
Kagera
Jeshi la polisi wilaya ya Kyerwa Mkoani Kagera limehitimisha rasmi fainali ya mchezo wa mpira wa miguu huku jeshi Hilo likiwataka wananchi kulipoti vitendo vya uharifu na kupinga ukatili wa kijinsia katika jamii.
Akizungumza na wananchi katika shamla shamla za fainali ya (Kyerwa jamii cup 2024) Mkuu wa polisi wilayani humo SSP Mohamed M.Mussa, amesema lengo la kuanzisha mashindano hayo ni kufichua waharifu na kupinga uharifu ,kuibua na kukemea matukio ya ukatili wa kijinsia katika jamii pamoja na jamii kushirikiana na polisi na polisi kuwa sehemu ya jamii.
"Sisi kama polisi hatuwezi kutokomeza vitendo vihovu na vya kiharifu katika jamii bila kushirikiana na jamii ambayo ni nyinyi hapa hivyo kuwa Hapa na kuanzisha michezo hii ni kuwahakikishia kuwa polisi ni kama nyie tu ila sisi tupo kuwasaidia na kusaidiana ili jamii zetu ziwe Bora na zenye ulinzi zaidi,naamini tukitoka hapa tusikae kimya pale tunapoona viashiria vibaya kwetu toeni taarifa sahihi na tunataka kyerwa yetu iwe imara zaidi,amesema SSP Mohamed "
Aidha nae Diwani wa kata Nkwenda Bw Edward Katunzi ameongeza kuwa michezo hasa mpira wa miguu ni Moja ya burudani kumbwa kwa vijana hasa katika kata yake hivyo na kusema kuwa atashiriki Kila hatua ikiwemo kutoa motisha ya zawadi kwa washiriki wote wa michezo hiyo pia na kuendelea kubuni vipaji vingine ili kila mwananchi wa Kyerwa hasa wa kata ya Nkwenda aweze kushiriki.
Pia nae Hamis Hassan Jumanne Mkurugenzi wa kuwanda Cha Kombucha ambaye ni Moja ya wadhamini wa mashindano hayo amesema kuwa wilaya ya Kyerwa inapakana na nchi jirani hivyo ni Bora zaidi kuendeleza michezo ili kudumisha urafiki,pia amewaomba wafanyabiashara wenzake kufanya juhudi zote za Serikali na kushiriki kazi za kijamii zaidi kwa sababu bidhaa wanazozalisha zinatumiwa na jamii.
Nae Mkuu wa wilaya hiyo ya Kyerwa Bi Zaitun abdallah Msofe ambaye alikuwa Mgeni rasmi katika fainali hiyo amesema wataendelea kuwa na ligi za mpira wa miguu katika kata zote za wilaya ya Kyerwa ili kuendeleza umoja na ushikamano,kuelimisha masuala mbalimbali ya jamii ,kujenga afya na Burudani kwa ujumla.
Mkuu huyo ametoa wito kwa vijana kushiriki mafunzo ya mgambo yanayoendelea wilayani humo na kuwataka wajiunge,na kusema kuwa wapo wanaosema hawana muda lakini mafunzo hayo yanafanyika mchana hivyo amewataka kufanya shughuli zao asubuhi na mchana kwenda kwenye mafunzo ili kuendeleza uzalendo na kujifunza namna ya kulinda mali za jamii na nchi kwa ujumla.
Hata hivyo Mwenyekiti wa chama Cha mpira wa miguu wilayani humo Bw Renatus Bonephace Kabila ametoa pongezi kwa waanzilishi wa mashindano hayo ya( POLISI JAMII CUP )huku akisema ni mashindano ya kwanza tangu kuanzishwa kwa wilaya hiyo na kusema kuwa mashindano hayo ya medumu ndani ya juma mbili kwa kushiriki timu mbalimbali,na kusema changamoto zinazowakabiri ni ukosefu wa uwanja Bora wa mpira wa miguu.
Katika fainali hiyo ziliweza kushiriki timu mbili za Karongo Fc na Nkwenda stand United huku Karongo ikiichapa Nkwenda bao 2 kwa 0 na michezo mingine iliyochezwa ni kuvuta kamba na kukimbiza kuku washiriki wakiwa ni Polisi jamii dhidi ya Watendaji wa kata na kauli mbiu katika michezo hiyo ikiwa ,( KYERWA POLISI JAMII CUP 2024,Familia yetu Haina Mharifu ).
0 Comments