Header Ads Widget

OJADACT YASHIRIKI MAANDHIMISHO YA KITAIFA YA KUPIGA VITA DAWA ZA KULEVYA

Na .Matukio Daima media 

Mwanza

Chama.cha Waandishi wa Habari wa Kupiga Vita Matumizi ya Dawa za Kulevya na Uhalifu Tanzania (OJADACT) kimeshiriki maadhimisho ya kitaifa ya kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya yaliyofanyika kwenye uwanja wa Nyamagana Jijini Dar es Salaam.


Mwenyekiti wa OJADACT Edwin Soko ameongoza  sekretarieti na wanachama wa OJADACT kwenye kushiriki maadhimisho hayo.


Edwin Soko amesema kuwa, maadhmisho ya mwaka huu yanabeba kauli mbiu ya wekeza kwenye kinga na tiba dhidi ya dawa za kulevya, ambayo inatoa jukumu kwenye kuhimiza kinga zaidi kwenye kukabiliana na athari za dawa za kulevya.

Soko amesema kuwa, Mkoa wa Mwanza  pia umekuwa miongoni mwa mikoa inayoathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya, hivyo kupitia maadhimsho ya mwaka huu ni wazi kuwa jitihada za dhati zinahitajika kwenye kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya.



Soko amewashukuru pia wanachama wa OJADACT na waandishi wa habari wote kwa kuwa mabalozi wazuri wa kuandika habari za dawa za kulevya na kulenga kutoa elimu ya  athari za dawa za kulevya Nchini.


Soko alibainisha kuwa OJADACT itaendelea kuwajengea uwezo waandishi wa habari kwenye kuripoti habari za dawa za kulevya.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI