Baada ya aliyekuwa Kada maarufu wa Chadema na Mwenyekiti mstaafu waxchama hicho Kanda ya Nyasa mchungaji Peter Msigwa kujiunga CCM ,mwenyekiti wa Chadema Taifa Freema Mbowe amevunja ukimya na kuandika ujumbe mzito .
Katika ukrasa wake wa X Mbowe ameandika hivi "Kuwa chama cha upinzani hasa CHADEMA sio suala jepesi, linahitaji ujasiri wa namna ya pekee.
Viongozi wengi wa upinzani na Watanzania wazalendo wa nchi hii wanapitia nyakati ngumu kutokana na uoga wa serikali ya CCM.
Marehemu Mzee Lowassa alithubutu kuingia CHADEMA, japo baada ya muda alirudi CCM tunatambua ujasiri wa maamuzi yake.
Kitu pekee kitakachiokoa Tanzania kutoka kwenye mikono ya watawala ni ujasiri na uthubutu wa mwananchi mmoja mmoja; tuanze sasa kulipigania taifa letu."
0 Comments