Header Ads Widget

SERIKALI IMETENGA FEDHA KWA AJILI YA UJENZI WA DARAJA

Na Hamida Ramadhan Matukio Daima App Dodoma


WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) Peramiho ameelekeza Wakala wa Barabara za Vijijini na Mjini (TARURA) Halmashauri ya wilaya ya Songea kuhakikisha daraja la Lumecha linajengwa ndani ya kipindi kifupi na kwa ubora.


Waziri ametoa kauli hiyo wakati wa ziara yake ya kutembelea Miradi ya maendeleo katika kijiji cha Liweta Halmashauri ya wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma.

“Serikali imetoa kiasi cha Millioni Mia nne kujenga Madaraja na akiba ya fedha itakayobaki itatumika kutengeneza barabara mpaka kijiji cha Liweta ikiwa ni pamoja na kufukia shimo lilopo katika barabara hiyo alisema,” Waziri Mhagama.


kazi ya ujenzi wa barabara ni kazi muhimu naomba wananchi msaidie katika kulinda mradi ili ujenzi ili ukamilike kwa wakati na tufungue njia zitakazochochea uchumia katika kijiji cha Liweta.



 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI