Mbunge wa Mbeya vijijini Oran Manasse Njeza, ameanza ziara katika vijiji na kata mbalimbali za jimbo la Mbeya vijijini ambapo ametembelea shule ya msingi Izumbwe II kata ya Iwiji na kuahidi kwa kushirikiana na Halmashauri ya Mbeya kuhakikisha fedha zinatafutwa ili kuiboresha kutokana na ukongwe wake.
Baada ya kutoka shuleni hapo, Mbunge Njeza amezungumza na wananchi wa kijiji cha Izumbwe akieleza yaliyofanyika na mipango endelevu kisha kutembelea shule ya msingi Sayuma na baadaye kwenda kuzungumza na wananchi wa Iwiji kupitia mkutano wa hadhara..
0 Comments