Na Matukio Daima Media, Mbeya
KATIKA kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa viongozi wa umoja wa wanawake mkoa wa Mbeya(UWT)kufanya usajili wa wanachama katika wilaya zao ili kupata wawakilishi wengi katika uchaguzi mkuu 2025.
Kauli hiyo imetolewa Julai 11,2024 na Naibu Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari (Mb) Mhandisi,Maryprisca Mahundi wakati wa kukabidhi simu janja 15 kwa viongozi wa UWT mkoa wa Mbeya.
"Kila ofisi ya wilaya itapata simu mbili pamoja na ofisi ya mkoa kwa ajili ya kuhamasisha wanawake wapate usajili wa kuwa wanachama wa UWT hii itasaidia kwenye uchaguzi mkuu tuweze kupata uwakilishi mwingi"amesema Mhandisi Mahundi.
Hata hivyo Mhandisi Mahundi amewataka wanawake hao kuhamasisha wanawake wenzao kujitokeza kwa wingi katika kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ikiwemo Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Vijiji ifikapo mwezi Novemba 2024.
Pamoja na kukabidhi simu hizo pia Mhandisi Mahundi alichangia Mil.10 kwa ajili ya Ujenzi wa ofisi ya Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Chunya ikiwa ni ahadi yake aliyokuwa ameitoa ya kuchangia Mil.27 ,sambamba na hayo alitoa kanga doti 72 kwa Wajumbe walioshiriki Baraza la Umoja wa Wanawake (UWT) wilayani Chunya.
0 Comments