Na Hamida Ramdhan,Matukio Daima Media Dodoma
MGOMBEA urais wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) Salum Ali Mwalimu ameahidi kama atakuwa Rais wa Tanzania atahakikisha Tanzania inapata katiba mpya pamoja na kufumua sheria zote ambazo watanzania wamekuwa na kiu nazo.
Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu,Mwalimu huku akiwa mgombea wa 11 amesema nchi inakwenda kupata Katiba mpya hivyo Bunge litakuwa lenye uhuru na mahakama yenye uhuru.
"Tunakwenda kuwa serikali inayoangali matakwa yawatu isiyo kulindana na vyombo vya habari kuwa huru viweze kutupia jicho na kusema, "amesema mgombea huyo.
Akiwa ameambatana na mgombea mwenza Devotha Minja amesema wana furaha kubwa bila kujali huko mbele kutatokea nini wanachojali historia itabadilika tanzania kuwa na Rais na Makamu wake wana habari
Amesema mabadiliko msingi wake ni kwenye katiba tutaenda kufanya serikali inayoangakia haki za watu nan kuwa huru
"Sasa tunakwenda kusaka wadhamini na Kampeni zetu tutaizindua Zanzibar tunaomba watanzania kutuamini tuwaongoze, ''Amessma
Na kuongeza "Tumefarijika sana na mapokezi ya dodoma naamini maeneo mengine tutapokelewa vizuri,"Amesema Mwalimu
Ameeleza kuwa ,wakati wa wambadiliko ni sasa nikishinda naingia na kuwa kiongozi msafi sina deni na sitaona aibu wala kumuonea mtu ibu kutokana na usafi wangu hivo nasema wazi sina jambo lolote nililowahi kulificha .
"Mimi na mgombea mwenzangu ni wasafi fikra zetu ni safi hakuna makandokando yoyote yatakayotuzuia kwenda kufanya mustakabaki wa taifa letu, "
Amesema Tumekulia maisha ya kimaskini tunawaelewa watanzania hivyo chama chetu tutawaondoa watanzania kwenye umaskini
Naye Mgombea Mwenza Devotha Minja anasema wa Tanzania wanauelewa tayari waneupima uwezo wa wananwake nakuzikubali
Amesema Watanzania wanaamini wanawake wakiwa kwenye nafasi za maamusi watawasiaida hususani kwenye masuala ya afya
"Wanawake wana uwezo wa kusukuma agenda za maji uzazi elimu na kuendelea kuvipigania hivyo vipaumbele , " Amesema
Na Kuongeza "Niwaombe watanzania kuendelea kuwaamini wanawake na kuto wadhihaki, " Amesema
0 Comments