Na Fadhili Abdallah,Kigoma
MBUNGE wa jimbo la Kigoma Kaskazini Assa Makanika amelitaka shirika hilo kuhakikisha umeme huo unafika vitongojini kwa wananchi ili waweze kuutumia kwa ajili ya kuinua shughuli zao za uzalishaji.
Makanika alisema hayo akihutubia mkutano wa hadhara kwenye Kijiji cha Bilate halmashauri ya wilaya Kigoma akiwa kwenye mfululizo wa ziara ya kutembelea na kuzungumza na wananchi wa jimbo hilo alisema kuwa uwepo wa umeme huo ni lazima ulete mabadiliko ya moja kwa moja kwa wananchi kuhakikisha unaboresha shughuli zao za uchumi na kuinua kipato chao.
Alisema kuwa wakati huu ambao serikali inatekeleza mradi mkubwa wa gridi ya taifa ni vizuri miradi ya umeme vijijini na vitongoji itekelezwe kwa ufanisi kwani bado sehemu kubwa ya jimbo hilo hakuna umeme kwenye vitongoji na kumekuwa na malalamiko makubwa ya wananchi wakihitaji uwepo wa umeme kwenye maeneo yao.
Akitoa ufafanuzi kwenye mkutano huo wa mbunge Mhandisi wa miradi ya Umeme vijijini kutoka TANESCO Kigoma, Mhandisi Fadhili Dello alisema kuwa bado vitongoji 75 katika jimbo hilo havijafikiwa na umeme na kuanzia August Mosi wanatarajia kuanza utekelezaji wa kupeleka umeme kwenye vitongoji ambapo mpango wa awali vitongoji 42 vitafikiwa, miradi 22 ya ujazilizi na miradi 12 ya maeneo ya pembeni ya miji ambapo wakandarasi watatu wamepangwa kutekeleza kazi hizo.
Mmoja wa wananchi hao, Ellius Paulo alisema kuwa kukosekana kwa umeme kunaathiri shughuli za uzalishaji za wananchi katika kuanzisha viwanda vidogo ikiwemo vya kuchakata mazao ya michikichi na mashine za kusaga kwa ajili ya kusindika unga kwa ajili ya biashara.
Mwisho.
0 Comments