Header Ads Widget

LUCY HAULE ADAIWA KUUWAWA NA MPENZI WAKE

 


JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limesema kuwa Mnamo tarehe 25 mwezi huu Majira ya 2024 saa 3:20 asubuh ilipata taarifa kuwa eno la Goba Matosa, Kinondoni kulikuwa na tukio la mauaji yaliyotokana na ugomvi kati ya watu wanaodaiwa kuwa ni wapenzi. 


Akiongea na waandishi wa habari Leo Muliro J. Muliro - SACP Kamanda Kanda Maalum ya Polisi

Amesema Polisi baada ya kufika eneo la tukio walibaini kuwepo kwa mwili wa mtu ambaye alishapoteza maisha aliyefahamika kwa jina la Lucy Stevin Haule(29) mfanyakazi wa kiwanda cha pombe kali iitwayo nguvu banana wine.


Aidha amesema uchunguzi wa awali umeonesha marehemu aliuawa na mpenzi wake aliyefahamika kwa jina la Musa Sasi (32) anayefanya kazi ya kibarua katika kiwanda cha pombe ya banana, na Mkazi wa Goba Matosa.



"Baada ya kumuua mpenzi wake, mtuhumiwa naye alijaribu kujiua kwa kutumia kisu, kwa kujichoma shingoni. Mtuhumiwa huyo amekamatwa na hali yake ni mbaya na yupo Hospitali ya rufaa ya Mwananyamala," Amesema Kamanda Muliro


Na kuongeza " Chanzo halisi cha ugomvi uliopelekea mauji hayo bado kinachunguzwa, " Amesema


Hata hivyo Jeshi la Polisi linatoa wito pindi watu wanapokuwa na migogoro au matatizo ya kijamii wazishirikishe taasisi mbalimbali za kisheria, za kiserikali na zisizo za kiserikali lakini pia taasisi za kidini ili zisaidie kutatua matatizo ya wahusika.


AmesemaVitendo vya ukatili ni pamoja na vya kubaka, kulawiti, kunajisi, mauaji, na ukiukwaji mwingine wowote wa sheria unaohusisha haki za watoto.


Amesema Tarehe 24 Julai, 2024 kupitia mitandao ya kijamii kumekuwa na taarifa zilizojaa sintofahamu kuhusu kipande cha picha ya video ikionesha kijana mmoja wa kiume kutoka eneo la Ilala Bungoni akihojiwa na wananchi kusiana jaribio la wizi wa mtoto.


"Baada ya kupata taarifa hizo Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam lilizifuatilia taarifa hizo na kubaini kwamba tukio la kipande hicho cha video sio mwaka huu au mwaka jana bali lilitokea Julai, 2022 eneo la Ilala Sharifu Shamba na kuripotiwa kituo cha Polisi Ilala/Pangani kwa madai ya mama moja kumtuhumu Frank Moi Chacha (18) mkazi wa Vingunguti kutaka kuiba mtoto wake, " Amesema 


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI