Header Ads Widget

KAMATI YA RUFAA YA ADC KUMALIZA MGOGORO, YAMPATANISHA DOYO NA ITUTU

 


Na Fatma Ally, Matukio DaimaApp

Kamati ya Rufaa ya Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC) imesema inatarajia kumaliza tofauti ndani ya siku 5 kati ya aliyekuwa mgombea wa nafasi ya Uenyekiti Doyo Hassan Doyo na Mwenyekiti wa chama hicho Shaaban Haji Itutu baada ya kukaa nao pamoja.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya rufaa Said Miraji Abdalla amesema kuwa kamati hiyo ilipokea barua ya rufaa kutoka kwa Doyo Hassan ndani ya saa 48 baada ya uchaguzi kumalizika ambayo ikieleza malalamiko juu ya uchaguzi huo kuwa na dosari .


Amesema kuwa, barua hiyo ilikua na malalamiko ya rufaa akiwa na hoja takriban saba ikiwemo ongezeko la wapiga kura, mkutano haukufuata sheria ya vyama vya siasa, wajumbe wa bodi ya uongozi Taifa hawakuchaguliwa bali waliteuliwa na msimamizi aliwazuia kufanya kampeni wakati wa uchaguzi.


Hata hivyo, amesema pamoja na mambo mengi pia miongoni mwa malalamiko yaliyotolewa ni pamoja na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Hamadi Rashid kuendelea na uenyekiti wa kikao cha uchaguzi hadi mwisho ikiwa ni kinyume na katiba na kanuni za ADC.


Ameongeza kuwa, rufaa ni haki ya kila mwenye malalamiko kwa mujibu wa kanuni za Chama hivyo baada ya uchaguzi Mkuu wa ADC ambao Shaaban Haji Itutu alitangazwa mshindi kwa kura 121 dhidi ya kura 70 za mpinzani wake Doyo Hassan Doyo hivyo Doyo kutumia haki yake ya msingi kukata rufaa.


"Rufaa ni haki ya kila mwanachama kwa mujibu wa katiba kati uchaguzi pia Katiba ya ADC inaruhusu wataalamu kuruhusiwa kuingia katika kamati kupitia kifungu cha 12 cha katiba hiyo, tulipokea rufaa ya Doyo tulimwandikia barua Itutu na yeye akatoa malalamiko yake kwa Doyo, sisi kama kamati tuliamua kuwaweka pamoja kufanya usulihishi" amesema Miraji.


Hata hivyo, amesema kamati iliwasilisha barua kwa upande wa walalamikiwa ambapo nao waliwasilisha pingamizi na kudai kuwa Doyo anafanya vikao na waandishi bila kusikiliza maamuzi ya kamati.


Ameongeza kuwa, walikutana na pande zote mbili na kufanya upatanisho kwanza na baadae kuendelea na kikao na kukubaliana kwamba wataendelea kulitatua swala hilo ndani ya chama na ambaye hataridhika na maamuzi ya ADC basi ataruhusiwa kuendelea kutafuta haki katika ngazi zinazofwata.


"Upatanisho na suluhu huleta umoja,amani na mshikamano katika taifa na jamii kwa pamoja hivyo maridhiano hayo yametoka na misingi sita ikiwemo katiba ya ADC, Amesisitiza na kuongeza kuwa,


Ameongeza "Tumeona maridhiano yanapokosekana huleta mfarakano ndani ya chama na tumeona katika vyama vya upinzani kila baada ya uchaguzi panatokea mtafaruko mfano katika vyama mbalimbali wakifarakana kwa kukosa maridhiano,tumeona katika chama cha CUF, CHADEMA wanachama wanahama na kwenda vyama vingine"


Sambamba na hayo, ametoa wito kwa vyama vingine kuunda kamati za rufaa na maridhiano zinazohusisha watu kutoka nje ya chama ili kuhakikisha kunakuwa na demokrasia ya kutosha katika maamuzi yote yanayofanyika.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI