Header Ads Widget

KUWENI NA UPENDO NA KUCHUKULIANA: MWALUNENGE.




Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Mbeya, Patrick Mwalunenge amewataka waumini wa kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania Dayosisi ya konde, Jimbo la Mbeya magharibi usharika wa forest kudumisha upendo na kuchukuliana kuliko kuwekeana visasi.


Mwalunenge ameyasema hayo wakati akiwa kanisani hapo kama mgemi rasmi katika harambee ya kuchangia ujenzi wa chuo cha afya na tiba kinacho tarajiwa kujengwa, ikiwa ni sehemu ya mradi wa kanisa.



Kupitia harambee hiyo Mwalunenge amechangia shilingi milioni 20, ambapo kusudio la harambee hiyo ni kupata shilingi milioni 150.


Jumla ya pesa iliyopatikana kupitia harambee hiyo ni zaidi ya shilingi milioni 156, kama ambavyo askofu mkuu wa kanisa hilo Tanzania Alex Malasusa alivyohitimisha.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI