Header Ads Widget

DIWANI KATA YA ISYESYE AWAPA MOTISHA WALIMU KWA KUFANYA VIZURI


Na Matukio Daima Media, Mbeya 



DIWANI wa kata ya Isyesye mkoani Mbeya,Ibra John amekabidhi sukari kilo 50  na majani ya chai kwa walimu wa  shule tatu za  msingi na Sekondari zilizopo katika kata hiyo zilizofaulisha kwa zaidi ya asilimia 90.


Diwani huyo ametaja shule zilizofanya vizuri kuwa ni Isyesye Sekondari,Ilomba shule ya msingi,Hayanga Shule ya msingi ikiwa ni sehemu ya motisha na kujali kazi kubwa iliyofanywa na walimu hao.


Motisha hiyo  ya sukari kilo 50 na majani ya shillingi 10,000  kwa kila shule  .


"Hii ni sehem ya mimi kama Diwani  kutambua mchango wao katika kuelimisha wananchi wa Isyesye na Taifa kwa jumla

Shule zetu hizi kwa mwaka huu zilifaulisha wanafunzi kwa zaidi ya 90% hivyo tunawapa pongezi sana na waendelee na juhudi hizo ktk majukum yao"amesema Diwani John 


Amesema kuwa kazi inayofanywa na walimu ni kubwa ni vema kutenga muda kuwashukuru hata kwa kidogo kinachopatikana ili kuwapa moyo wa ufanyaji kazi kwa bidii 


 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI