Header Ads Widget

WAZAZI NA WALEZI WATAKIWA KUSHIRIKI KATIKA UJENZI WA CHUO CHA VETA ARUMERU

 


Na,Jusline Marco;Dodoma

Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Mhe.John Danielson Palangyo amewataka wananchi wa Kata ya Uwiro Wilayani Arumeru Mkoani Arusha kutumia fursa ya kupata elimu ya ufudi pindi chuo cha VETA kinachojengwa katika Kata hiyo kitakapo kamilika ikiwa ni sambamba na kushiriki katika ujenzi wa chuo hicjo na utunzaji wa miundombimu hiyo.



Akizungumza nje ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kuuliza swali kwa Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Omary Kipanga akitaka kufahaku ni lini serikali itakamilisha ujenzi wa chuo cha VETA katika Kata ya Uwiro Wilayani Aruameru.



Mhe.Palangyo ameishuruku serikali kwa hatua iliyofikia ya ujenzi wa chuo hicho ambapo amesema uwepo wa chuo hicho Wilayani humo kwanza kitatoa ajira, pili kitatoa fursa kwa wananchi kupata elimu ya ufundi kwani elimu ya ufundi ni nyenzo muhimu katika maendeleo ya nchi ambapo ametoa wito kwa wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao kuoata elimu hiyo kwa maendeleo yao binafsi na jimbo kwa ujumla. 



Akijibu swali hilo Mhe.Kipanga Naibu Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia a4mesema katika mwaka wa fedha 2023/24 serikali imekamilisha ujenzi wa vyuo 25 vya veta vya Wilaya pamoja na vyuo 4 vya Veta vya Mikoa ambapo amesema melengo ya serikai hadi kufika mwezi wa kumi mwaka huu vyote vyote vya veta vinavuojengwa viwe vimekamilika katika awamu ya kwanza kusudi mwezi Novemba mwaka huu waweze kuanza kutoa kozi za muda mfupi na mwezi Januari 2025 kuanza kutoa kozi za muda mrefu.



Awali Mhe.Palangyo akizungumzia uwepo wa michango mingi katika shule za serikali Mhe.Palangyo amesema kuwa ni vyema wakuu wa shule na wakurugenzi wa halmashauri wakazingatia kauli ya serikali ya kutozidisha kiwango cha michango cha shilingi elfu 80 kwa shule za bweni na elfu 59 kwa shile za kutwa.



Naibu Waziri Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe.Zainabu Katimba akijibu swali la Mbunge wa Konde Mohamed Issa aliyetaka kujua mipango ya serikali katika kuleta unafuu wa gharama za michango ya kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza na tano ambapo amesema serikali imeagiza kupokelewa kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa kuzingatia Waraka wa Elimu Na.3 wa mwaka 2016 wa elimu msingi bila ada unaowataka wanafunzi kutotoa michango yoyote bila kibali cha Wakuu wa Wilaya.



Aidha ameongeza kuwa serikali imetoa maelekezo ya kujiunga na kidato cha tano katika shule zote za sekondari za serikali ambapo ukomo wa michango hiyo umebainishwa kuwa ni shilingi 80000 kwa shule za bweni na shilingi 50000 kwa shule za kutwa ili kuweza kuleta unafuu wa gharama za michango.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI