Na WILLIUM PAUL.
SERIKALI imezitaka kampuni za mawasiliano zilizopewa kazi ya kujenga minara ya mawasiliano kutekeleza kazi hizo kwa wakati.
Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya habari, Maryprisca Mahundi wakati akijibu swali la Mbunge wa jimbo la Moshi vijijini, Prof. Patrick Ndakidemi alilohoji Kampuni ya simu ya Tigo ilishinda zabuni ya kujenga mnara wa mawasiliano katika Kata ya Uru Shimbwe, lakini hadi sasa utekelezaji wa mradi huo umesuasua sana.
Je Serikali ina mikakati gani ya kusimamia utekelezaji wa mradi huu.
Naibu Waziri Maryprisca alimpongeza Mbunge Prof. Ndakidemi kwa kuwa mfuatiliaji wa jambo hilo na kutoa wito kwa makampuni yote ya mawasiliano ambayo yamepewa kazi kuwa wanahitaji kuona kazi zikifanyika kwa wakati na kuahidi kuhakikisha anafwatilia na kusimamia mwenyewe kazi hiyo.
Mwisho..
0 Comments