Header Ads Widget

WANANCHI KAGERA WAOMBWA KUJITOKEZA KUPOKEA MWENGE

 


Na Matukio Daima App.

Kagera 

Wanachi Mkoa Kagera wameshauriwa kujitokeza kwa wingi kuupokea Mwenge wa Uhuru pindi ukifika ndani ya Mkoa Kagera.

Akizungumza na wakuu wa wilaya ,Wakurugenzi pamoja wasimamizi wa miradi ya maendeleo katika nyakati tofauti ndani ya Halmashauri zao Mtaalamu na Mshauri wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Bi Hellen Mbezi amesema kwa Sasa Kila mwenye nafasi na mshiriki wa Mwenge wa Uhuru ni jukumu lake kuendelea kuwaelimisha wananchi juu ya ujio wa Mwenge wa Uhuru.



"Jamani hivi karibuni tuna ujio wa Mgeni na Mgeni huyo ni Mwenge wa Uhuru toeni elimu kwa Kila mwanchi ajue umuhimu na kazi haswa za Mwenge wa Uhuru,na namna nzuri ya wao kuweza  kushiriki siku hiyo,amesema Bi Hellen"


Adha,amesema katika Moja ya  kazi za Mbio za  Mwenge ni kukagua ,kutembelea,kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi ya maendeleo hivyo ni vema kufuata taratibu za utekelezaji  Bora wa miradi  hiyo.


Pia Bi Hellen amesisitiza  kutoa elimu katika jamii juu ya magojwa ya Ukimwi (VVU),Malaria,Kipindupindu ili kupunguza maambukizi ya Magonjwa hayo pamoja na mapambano dhidi ya rushwa.


Hata hivyo amezitaja kazi nyingine zinazotakiwa kufanyika katika Mbio hizo za Mwenge wa Uhuru kuwa ni Upandaji wa miti,Utoaji wa damu salama, lishe na  huduma nyingine za kiafya.


Naye Mratibu Msaidizi wa Mwenge wa Uhuru  Mkoa Kagera Bw Yasin Mwinory ameongeza kuwa kwa Sasa Mkoa upo katika Mwendelezo wa Maandalizi ya Mapokezi  ya Mwenge wa Uhuru hivyo ni wajibu wake kuzitembelea Halmashauri zote za Mkoa Kagera kwa ajili ya kushauri na kuona namna nzuri ya kuibuka kidedea katika Mbio hizo.



Ikumbukwe kuwa Mwenge wa Uhuru unatalajia kuwasili ndani ya Mkoa Kagera mnamo September 22, 2024.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI