AJALI:Abiria zaidi ya 45 waliokuwa wakisafiri na basi la kampuni ya Upendo kutoka Iringa mjini Kuelekea Tungamalenga wilaya ya Iringa Vijijini wamenusurika Kifo baada ya basi hilo kupinduka katika barabara kuu ya Iringa -Tungamalenga.
Mashuhuda wa tukio Hilo wameueleza mtandao wa Matukio Daima media kuwa ajali hiyo imetokea Asubuhi Mlima Ipwasi na chanzo ni ubovu wa Basi .
Walisema hakuna Kifo zaidi ya Majeruhi .
Matukio Daima media tunaendelea kumtafuta kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa ili kupata undani wa taarifa hii.
0 Comments