Header Ads Widget

WAKILI MWABUKUSI AAHIDI KUMSINDIKIZA MPINA KWENYE KAMATI YA MAADILI.

Mwanaharakati na mwambata wa Sauti ya wa-Tanzania Wakili Boniface Anyisile Mwabukusi, amesema atamsindikiza bungeni Mbunge wa Jimbo la Kisesa Mhe.Luhaga Mpina atakapowasili kwa ajili ya tuhuma zinazomkabili kama alivyoagizwa na Spika wa Bunge Dkt.Tulia Ackson.


Wakili Boniface Mwabukusi amesema Mpina amekuwa Mbunge anayesimama kidete kutetea maslahi ya Taifa hivyo hoja alizozitoa kwa mtazamo wake ni kwa ajili ya manufaa ya wa-Tanzania.


Amesema Kilimo ni uti wa mgongo kwa kuajiri zaidi ya asilimia themanini ya wananchi hivyo lazima Wizara chini ya Waziri wake Hussein Bashe isimame imara na kutoa takwimu sawa kama alivyoeleza kwa uthibitisho Mbunge Mpina.


Wakili huyo mwenyeji wa mkoani Mbeya, ameeleza kumshangaa Spika wa Bunge la Tanzania Dkt. Tulia Ackson kumpeleka kwenye kamati ya maadili ya Bunge akidaiwa kulikosea Bunge badala ya kuunda kamati maalum ya kubaini mambo yaliyowasilishwa na Mbunge huyo ikiwemo bei kubwa ya sukari.


Mbunge wa Kisesa mkoani Simiyu Mhe. Luaga Mpina ambaye amewahi kuwa Waziri wa Mifugo na uvuvi, amekuwa Mbunge anayehoji masuala mbalimbali ya kijimbo na kitaifa katika kuhakikisha Serikali inawajibika na kuyashughulikia kwa maslahi ya umma hali inayoonekana kwa baadhi ya watu kana kwamba ni kukosa utiifu na nidhamu hivyo kukosolewa na makundi ya watu mbalimbali huku baadhi yao wakiwemo wapinzani wakimuunga mkono katika harakati zake za kuwapigania wananchi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI